Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 9
  • Nuhu Anajenga Safina

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nuhu Anajenga Safina
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Safina ya Noa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • “Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”
    Igeni Imani Yao
  • “Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Maji Yachukua Ulimwengu
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 9
Nuhu na familia yake wakileta wanyama na vyakula kwenye safina

HADITHI YA 9

Nuhu Anajenga Safina

NUHU alikuwa na mke na wana watatu. Wana hao ni Shemu, Hamu na Yafeti. Kila mmoja wao alikuwa na mke. Kwa hiyo, jamaa ya Nuhu ilikuwa yenye watu nane.

Mungu akamwagiza Nuhu afanye jambo geni. Alimwambia ajenge safina kubwa. Safina hiyo ilikuwa kubwa kama meli, lakini ilionekana kama sanduku kubwa, refu. ‘Fanya iwe urefu wa vyumba vitatu kwenda juu,’ Mungu akasema, ‘uweke nyumba ndani yake.’ Vyumba hivyo vilikuwa vya Nuhu na jamaa yake, wanyama, na chakula chao.

Tena Mungu akamwambia Nuhu aikaze safina hiyo ili maji yasiweze kuingia. Mungu akasema: ‘Nitaleta gharika kubwa iharibu ulimwengu mzima. Kila mtu nje ya safina atakufa.’

Nuhu na wanawe walimtii Yehova wakaanza kujenga safina. Lakini watu wengine walikuwa wakicheka tu. Walizidi kuwa wabaya.

Watu wanamcheka Nuhu anapowaambia kuhusu gharika itakayokuja

Kujenga safina kulichukua muda mrefu kwa sababu ilikuwa kubwa mno. Baada ya miaka mingi, ikamalizika. Kisha Mungu akamwambia Nuhu aingize wanyama katika safina. Tena Mungu alimwambia Nuhu aingize namna zote mbalimbali za ndege. Nuhu akafanya kama Mungu alivyosema.

Kisha, Nuhu na jamaa yake wakaingia katika safina. Ndipo Mungu akaufunga mlango. Nuhu na jamaa yake walingoja humo ndani. Je! kweli gharika ingekuja kama vile Mungu alivyosema?

Mwanzo 6:9-22; 7:1-9.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki