Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • my hadithi 15
  • Mke wa Lutu Alitazama Nyuma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mke wa Lutu Alitazama Nyuma
  • Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Mkumbuke Mke wa Loti
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Tayarisha kwa Ajili ya Kukombolewa Kuingia Ndani ya Ulimwengu Mpya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Mungu Afanya Agano na Abrahamu
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
  • Wasaidie Wengine Kukabiliana na Mkazo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
Pata Habari Zaidi
Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
my hadithi 15
Mke wa Lutu alitazama nyuma kuangalia Sodoma naye akawa nguzo ya chumvi

HADITHI YA 15

Mke wa Lutu Alitazama Nyuma

LUTU na jamaa yake walikaa Kanaani pamoja na Ibrahimu. Siku moja Ibrahimu alimwambia Lutu hivi: ‘Hapa hapana nchi ya kufaa wanyama wetu wote. Tafadhali, tutengane. Ukienda huku, na mimi nitakwenda kule.’

Lutu akaitazama nchi. Akaona sehemu ya nchi iliyo nzuri sana yenye maji na majani mazuri mengi ya wanyama wake. Hiyo ilikuwa Wilaya ya Yordani. Basi Lutu alipeleka jamaa yake na wanyama huko. Mwishowe wakakaa katika mji wa Sodoma.

Watu wa Sodoma walikuwa wabaya sana. Lutu alisumbuliwa, maana alikuwa mtu mzuri. Hata Mungu alisumbuliwa. Mwishowe, Mungu alituma malaika wawili wakamwonye Lutu kwamba Mungu ataharibu Sodoma, na Gomora mji wa karibu, maana ni miji mibaya.

Malaika hao wakamwambia Lutu hivi: ‘Fanya haraka! Chukua mke wako na binti zako wawili mwondoke huku!’ Malaika mmoja alisema: ‘Kimbieni mponye uhai wenu! Msitazame nyuma. Kimbieni kwenye mlima msiuawe.’

Lutu na binti zake wanakimbia kutoka Sodoma wakiwa wametazama mbele

Lutu na binti zake walitii, wakatoka Sodoma. Lakini mke wa Lutu hakutii. Walipokwisha kutembea mwendo fulani kutoka Sodoma, mke alisimama akatazama nyuma, akawa nguzo ya chumvi. Unaweza kumwona katika picha?

Tunaweza kujifunza somo zuri kwa hayo. Yanatuonyesha kwamba Mungu anaokoa wale wanaomtii, lakini wale wasiomtii watapoteza uhai wao.

Mwanzo 13:5-13; 18:20-33; 19:1-29; Luka 17:28-32; 2 Petro 2:6-8.

Maswali ya Funzo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki