Mifano na Masimulizi ya Kiunabii ya Watu Wanaoishi Sasa Watakaoirithi Milki ya Kidunia ya Ufalme wa Mungu
Walifananishwa na vikundi au watu mmoja mmoja wafuatao:
(1) Wana wa Noa na binti-wakwe zake (Mwanzo 6-9).
(2) Loti na binti zake (Mwanzo 19).
(3) Ndugu kumi wenye kutubu wa Yosefu (Mwanzo 37, 42-45).
(4) Wamisri wenye kupatwa na njaa kuu waliojiuza wenyewe kwa Yosefu (Mwanzo 41; 47:13-26).
(5) Kundi la watu waliochangamana lililotoka Misri pamoja na Waisraeli (Kutoka 12:38).
(6) Makabila kumi na mawili ya Israeli yasiyo ya Kilawi Siku ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 16; Mathayo 19:28).
(7) Wakaaji wa kigeni katika Israeli (Mambo ya Walawi 19:34).
(8) Hobabu yule shemeji ya Musa (Hesabu 10:29-32).
(9) Rahabu wa Yeriko (Yoshua 2, 6).
(10) Wagibeoni waliotafuta amani pamoja na Israeli (Yoshua 9, 10).
(11) Yaeli mke wa Heberi Mkeni (Waamuzi 4, 5).
(12) Yonathani mwana wa Mfalme Sauli (1 Samweli 18; 23:16, 17).
(13) Wageni waliopigana wakiwa pamoja na Daudi (2 Samweli 15:18-22).
(14) Malkia wa Sheba (1 Wafalme 10).
(15) Naamani aliyesafishwa ukoma (2 Wafalme 5).
(16) Yehonadabu mwana wa Rekabu (2 Wafalme 10:15-28).
(17) Wageni waliosali kuelekea hekalu la Yehova (2 Mambo ya Nyakati 6:32, 33).
(18) Wanethini na wana wa watumishi wa Sulemani wasio Waisraeli (Ezra 2, 8).
(19) Warekabi (Yeremia 35).
(20) Ebedmeleki Mwethiopia (Yeremia 38; 39:16-18).
(21) Waninewi waliotubu (Yona 3).
Tena, wanasimuliwa kiunabii kama ifuatavyo:
(1) Jamaa za ardhi zinazojibariki kupitia Abrahamu kwa njia ya mbegu yake (Mwanzo 12:3; 22:18).
(2) Mataifa yanayofurahi pamoja na watu wa Yehova (Kumbukumbu la Torati 32:43).
(3) Waadilifu, wale wanaomtumainia Yehova (Zaburi 37:9, 29).
(4) Wanawali wenzi wa bibi-arusi (Zaburi 45:14).
(5) Wanyofu na wasio na lawama (Mithali 2:21).
(6) Mataifa yanayofundishwa katika nyumba ya Yehova na wanaotembea katika mapito yake (Isaya 2:2-4).
(7) Mataifa yanayokuja kuulizia-ulizia kwenye ile Ishara (Isaya 11:10).
(8) Mataifa yanayotoka katika giza (Isaya 49:6, 9, 10).
(9) Taifa lisilojulikana zamani (Isaya 55:5).
(10) Wageni wanaohudumia Yehova na kulipenda jina lake (Isaya 56:6)
(11) “Wingi wa bahari,” “utajiri wa mataifa,” wale wanaokuja ‘wakiruka kama wingu la njiwa’ (Isaya 60:5, 6, 8).
(12) Wageni wanaochunga makundi ya kondoo ya Israeli, wageni walio wakulima na watunza mizabibu yake (Isaya 61:5).
(13) Wale wenye kutiwa alama katika kipaji cha uso na yule mwanamume mwenye kidau cha wino cha mwandishi (Ezekieli 9).
(14) Watu wanaoliitia jina la Yehova na kuokoka katika siku yake yenye kutia woga (Yoeli 2:32).
(15) Vitu vinavyotamanika vya mataifa yote (Hagai 2:7).
(16) Mataifa ‘yanayojiunga na Yehova’ (Zekaria 2:11).
(17) ‘Wanaume kumi wanaoshika rinda la Myahudi’ (Zekaria 8:23).
(18) Mataifa ambayo Mfalme anasema kwao amani (Zekaria 9:10).
(19) “Kondoo” wanaotendea ndugu za Mfalme mema (Mathayo 25:31-46).
(20) Mwana mpotevu aliyetubu (Luka 15:11-32).
(21) “Kondoo wengine” wanaosikiliza sauti ya Mchungaji Mwema (Yohana 10:16).
(22) Watu wanaomwamini Kristo na ‘hawatakufa kamwe’ (Yohana 11:26).
(23) Uumbaji utakaowekwa huru utoke katika utumwa na uchafu uwe na uhuru wa watoto wa Mungu (Warumi 8:20, 21).
(24) Wale wa ulimwengu watakaopata uzima wa milele kwa sababu ya kumwamini Mwana wa Mungu (1 Yohana 2:2; Yohana 3:16, 36).
(25) “Mkutano mkubwa” unaotumikia mchana na usiku katika hekalu la Yehova (Ufunuo 7:9-17).
(26) Ye yote anayekunywa maji ya uzima kisha yeye mwenyewe anawaambia wengine, “Njoo!” (Ufunuo 22:17).
Walioorodheshwa juu ni wale tu wanaozungumzwa au kutajwa katika kitabu hiki.