Wimbo Na. 142
Kuwahubiria Watu wa Namna Zote
Tunatamani kumwiga Mungu,
Kwa kuwa ye hana ubaguzi.
Awakaribisha watu kwake;
Kusudi awaokoe wote.
(KORASI)
Hatubagui mtu;
Popote atokapo.
Ujumbe wa Mungu twapa wote.
Kwa kuwa twawajali,
Twawaalika watu wa
namna zote waje kwa Mungu.
Hatujali wapatikanapo
Au jinsi waonekanavyo.
Jambo kuu ni jinsi walivyo—
Moyoni—Yule mtu wa ndani.
(KORASI)
Hatubagui mtu;
Popote atokapo.
Ujumbe wa Mungu twapa wote.
Kwa kuwa twawajali,
Twawaalika watu wa
namna zote waje kwa Mungu.
Yehova akaribisha wote
Waache njia za ulimwengu.
Tunataka kuwahubiria,
Watu wa aina zote waje.
(KORASI)
Hatubagui mtu;
Popote atokapo.
Ujumbe wa Mungu twapa wote.
Kwa kuwa twawajali,
Twawaalika watu wa
namna zote waje kwa Mungu.
(Ona pia Yoh. 12:32; Mdo. 10:34; 1 Tim. 4:10; Tit. 2:11.)