Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 88 uku. 206
  • Yesu Akamatwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Akamatwa
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Kristo Asalitiwa na Kukamatwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kusalitiwa na Kukamatwa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Kusalitiwa na Kukamatwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Yesu Katika Bustani
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 88 uku. 206
Yuda akimsaliti Yesu katika bustani ya Gethsemane

SOMO LA 88

Yesu Akamatwa

Yesu na mitume wake walitembea katika Bonde la Kidroni wakienda kwenye Mlima wa Mizeituni. Ilikuwa ni usiku na mwezi ulikuwa mpevu kabisa. Walipofika katika bustani ya Gethsemane, Yesu aliwaambia hivi: “Kaeni hapa na mwendelee kukesha.” Kisha, akaenda mbele kidogo katika bustani na kupiga magoti. Akiwa na uchungu mwingi alisali hivi kwa Yehova: “Acha mapenzi yako yatendeke.” Kisha, Yehova akamtuma malaika ili amwimarishe Yesu. Yesu aliporudi kwa mitume, alikuta watatu kati yao wakiwa wamelala. Akawaambia hivi: ‘Amkeni! Huu si wakati wa ninyi kulala! Saa imefika ya mimi kutiwa katika mikono ya adui zangu.’

Yuda anapewa mfuko wa pesa

Muda mfupi baadaye, Yuda alikuja akiwa na kundi kubwa la watu wenye mapanga na marungu. Alikuwa anajua mahali ambapo Yesu anaweza kupatikana kwa sababu walizoea kuja naye katika bustani hiyo mara kwa mara. Yuda alikuwa amewaambia askari kwamba atawaonyesha Yesu. Hivyo, alienda moja kwa moja kwa Yesu na kusema: ‘Habari, Mwalimu,’ na kisha, akambusu. Yesu akamuuliza: ‘Yuda unanisaliti kwa kunibusu?’

Yesu akasogea mbele na kuuliza umati huo hivi: “Mnamtafuta nani?” Wakasema: “Yesu Mnazareti.” Akawajibu: “Mimi ndiye,” na mara moja wanaume hao wakarudi nyuma na kuanguka chini. Kwa mara nyingine Yesu akawauliza: “Mnamtafuta nani?” Wakamjibu: “Yesu Mnazareti.” Yesu akawajibu: ‘Nimewaambia mimi ndiye. Waacheni hawa waende zao.’

Petro alipoona kile kilichokuwa kikiendelea, alichomoa upanga wake na kukata sikio la Malko, mtumishi wa kuhani mkuu. Lakini Yesu akagusa sikio la mwanamume huyo na kumponya. Kisha, akamwambia Petro hivi: ‘Rudisha upanga wako mahali pake. Ukipigana kwa upanga, utakufa kwa upanga.’ Askari wakamkamata Yesu na kumfunga mikono, lakini mitume wakakimbia. Kisha, umati ukampeleka Yesu kwa Anasi. Anasi alimhoji Yesu, halafu akamtuma kwa Kayafa aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka huo. Lakini ni nini kilichotokea kwa mitume?

“Ulimwenguni mtapata dhiki, lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu.”—Yohana 16:33

Maswali: Ni nini kilichotukia katika bustani ya Gethsemane? Unaweza kujifunza nini kutokana na mambo ambayo Yesu alifanya usiku huo?

Mathayo 26:36-57; Marko 14:32-50; Luka 22:39-54; Yohana 18:1-14, 19-24

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki