Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 89 uku. 208-uku. 209 fu. 1
  • Petro Anamkana Yesu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Petro Anamkana Yesu
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Kayafa Alikuwa Mpinzani Mkali wa Ibada ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Kuhani Mkuu Aliyemhukumu Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Akanwa Nyumbani kwa Kayafa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yesu Apelekwa kwa Anasi, Kisha kwa Kayafa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 89 uku. 208-uku. 209 fu. 1
Petro akimkana Yesu, katika ua wa nyumba ya Kayafa

SOMO LA 89

Petro Anamkana Yesu

Yesu alipokuwa na mitume wake katika chumba cha juu, aliwaambia hivi: ‘Usiku wa leo, ninyi nyote mtanikimbia.’ Petro akasema: ‘Sitakuacha! Hata ikiwa wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.’ Lakini Yesu akamwambia hivi: ‘Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu.’

Askari walipomchukua Yesu na kumpeleka kwa Kayafa, wengi kati ya mitume walikimbia. Hata hivyo, mitume wawili waliufuata umati kwa nyuma. Mmoja kati yao alikuwa Petro. Aliingia katika ua wa nyumba ya Kayafa na kuanza kuota moto. Kwa sababu ya mwanga wa moto, kijakazi mmoja alimwona Petro na kumwambia: ‘Ninakujua! Wewe ulikuwa pamoja na Yesu!’

Petro akamjibu: “Simjui wala sielewi unachosema.” Kisha, akatoka na kuelekea nje ya ua. Lakini baada ya muda kijakazi mwingine akamwona na kuuambia umati wa watu hivi: ‘Mtu huyu alikuwa pamoja na Yesu!’ Petro akajibu: ‘Mimi hata simjui Yesu!’ Mwanamume mwingine akasema: ‘Wewe ulikuwa pamoja naye! Njia yako ya kuzungumza inaonyesha kwamba wewe ni Mgalilaya, kama Yesu.’ Lakini Petro akaapa na kusema: ‘Simjui mtu huyo!’

Wakati huohuo, jogoo akawika. Petro akamwona Yesu akigeuka na kumtazama. Akayakumbuka maneno ya Yesu, halafu akatoka nje na kulia kwa uchungu.

Mambo hayo yalipokuwa yakiendelea, Sanhedrini iliamua kusikiliza kesi ya Yesu katika nyumba ya Kayafa. Walikuwa wameamua kwamba watamuua Yesu, sasa walikuwa wanamtafutia kosa. Hata hivyo, hawakupata kosa lolote dhidi yake. Mwishowe, Kayafa akamuuliza Yesu hivi moja kwa moja: ‘Je, wewe ni Mwana wa Mungu?’ Yesu akajibu: ‘Ndiyo.’ Kayafa akasema: ‘Amekufuru! Hatuhitaji ushahidi wa ziada.’ Kisha, wote wakakubaliana kwamba, ‘mtu huyu anastahili kufa.’ Wakampiga makofi, wakamtemea mate, na kumfunika usoni wakisema: ‘Ikiwa wewe ni nabii, tuambie ni nani aliyekupiga!’

Kulipopambazuka, walimchukua Yesu na kumpeleka katika Sanhedrini, kisha wakamuuliza hivi: ‘Je, wewe ni Mwana wa Mungu?’ Yesu akawajibu: ‘Ninyi mnasema kwamba mimi ndiye.’ Wakamhukumu kuwa na hatia ya kukufuru na baadaye wakampeleka kwa Pontio Pilato, Gavana wa Roma. Ni nini kilichotukia baada ya hapo? Acha tuone.

“Saa inakuja . . . wakati kila mmoja wenu atatawanyika na kwenda nyumbani kwake, nanyi mtaniacha peke yangu. Lakini siko peke yangu, kwa sababu Baba yuko pamoja nami.”​—Yohana 16:32

Maswali: Ni nini kilichotokea katika ua wa nyumba ya Kayafa? Kwa nini mahakama iliamua kumhukumu Yesu kifo?

Mathayo 26:31-35, 57–27:2; Marko 14:27-31, 53–15:1; Luka 22:55-71; Yohana 13:36-38; 18:15-18, 25-28

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki