WIMBO NA. 121
Tunahitaji Sifa ya Kujizuia
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova kwa moyo twakupenda;
Hata hivyo sisi dhambi twatenda.
Ya kimwili tusikazie.
Ya kiroho tuzingatie.
2. Twajaribiwa naye Shetani.
Na sheria ya dhambi imo ndani.
Neno Lako linatulinda.
Tuna hakika tutashinda.
3. Kwa neno na tendo tukusifu,
Jina lako kuu tusikashifu.
Mambo yote tuzingatie.
Sikuzote tujizuie.
(Ona pia 1 Kor. 9:25; Gal. 5:23; 2 Pet. 1:6.)