Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • it uku. 622
  • Ibilisi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ibilisi
  • Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Habari Zinazolingana
  • Usimpe Ibilisi Nafasi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Jihadhari na Adui Yako, Ibilisi!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
    Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia
Ufahamu wa Kina wa Maandiko
it uku. 622

IBILISI

Jina linalomfafanua Shetani kwa sababu ndiye mchongezi mkuu wa kwanza na mshtaki anayesema uwongo kumhusu Yehova, neno lake jema, na jina lake takatifu. Neno la Kigiriki di·aʹbo·los linamaanisha “mchongezi.” (Linganisha Lu 16:1, ambapo kitenzi kinachohusiana na neno di·a·balʹlo hutajwa.)​—Ona SHETANI.

Kwa karne nyingi Ibilisi amejidhihirisha kuwa mpinzani mkuu wa Mungu na wanadamu. Alibishana na Mikaeli kuhusu mwili wa Musa (Yud 9); alionyesha kwamba ana nguvu za kuwanasa wanadamu (1Ti 3:7; 2Ti 2:26); alitumia watu kama vile viongozi wa dini za uwongo, Yuda Iskariote, na Bar-Yesu kama watoto wake (Yoh 8:44; 13:2; Mdo 13:6, 10); aliwakandamiza watu hivi kwamba hawangeweza kuponywa na madaktari (Mdo 10:38); alihakikisha kwamba waadilifu wanatupwa gerezani (Ufu 2:10); na hata ana uwezo wa kusababisha kifo bila kutarajia (Ebr 2:14). Hivyo, Wakristo wanahimizwa kutompa Mchongezi huyu wa Mungu nafasi kwa kutoendelea kuwa na hasira. (Efe 4:27) Petro anaonya hivi: “Tunzeni akili zenu, iweni waangalifu! Adui yenu, Ibilisi, anatembea huku na huku kama simba anayenguruma, akitafuta kummeza mtu.”​—1Pe 5:8.

Kuna pindi nyingine katika maandishi ya awali ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo ambapo neno di·aʹbo·los huonekana lakini halirejelei Shetani, hivyo kwa kufaa neno hilo hutafsiriwa “mchongezi.” Kwa mfano, anapomrejelea Yuda, Yesu aliwaambia wale 12, “mmoja wenu ni mchongezi” (Yoh 6:70); wanawake kutanikoni walionywa kutokuwa wachongezi (1Ti 3:11; Tit 2:3); na kwamba “watu watakuwa . . . wachongezi” kama ishara mojawapo ya “siku za mwisho.”​—2Ti 3:1-5.

Sheria ya Yehova aliyowapa Waisraeli iliwakataza kuwa wachongezi. (Law 19:16) Kwa ujumla, Biblia inapinga vikali matumizi mabaya kama hayo ya ulimi.​—2Sa 19:27; Zb 15:3; 101:5; Met 11:13; 20:19; 30:10; Yer 6:28; 9:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki