Sababu Gani Kuchukua Wajibu kwa Uzito?
KATI ya wajibu ambao watu wengi leo wanashindwa kuchukua kwa uzito ni ule wa kulipa kodi. Kushindwa kutimiza wajibu wa mtu wa kodi kunajulikana kama “kuepa kodi.” Kulingana na aliyekuwa afisa wa kodi, “kuepa kodi kunakubalika kwa watu wengi. Watu wengi wanafikiri ni uhalifu wa kufurahisha.”
Kwa kadiri ionekanavyo watu wengi leo wanajaribu kumhakikisha Benjamin Franklin kuwa mwenye kosa aliposema: “Katika ulimwengu huu hakuna jambo la lazima isipokuwa kifo na kodi.” Kati ya mifano inayojulikana zaidi ya watu kama hao ni aliyekuwa makamu wa rais wa mojawapo la mashirika makubwa ya chuma ya Amerika. Kwa miaka 23 hakulipa hata kodi; kutojali ambako kulimgharimu karibu shilingi 490,000 za kodi za nyuma, hukumu na faini. Mbaya hata zaidi hakuwa mwingine ila aliyekuwa United States Commissioner of Internal Revenue, mtoza kodi mkuu wa taifa. Alishindwa kutoa habari ya shilingi 1,120,000 alizochuma, kwa sababu yake akatozwa faini ya shilingi 105,000 na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano.
Kuna ulegevu katika kujitwalia wajibu wa mtu katika shughuli zote za kibinadamu—kodi ni sehemu moja. Hivyo gazeti lijulikanalo sana la Kiamerika juu ya ‘nyumba na shamba’ lililalamika kwamba leo hakuna anayejali, hakuna anayechukua wajibu kwa uzito: “Tunatafuta raha yetu wenyewe na faida. . . . Kazi zinaharibika. Ni vigumu kumpata fundi wa kurekebisha vitu atakayefanya kazi nzuri mara ya kwanza. . . . Vitu vipya ghali vinapoteza mipini na vifungo kama vitu ovyo ovyo. Watumishi (kama wa hotelini) wanasingizia kukutumikia. Wafanya biashara wanapiga domo unaposubiri. Maafisi ya madaktari yanapanga maafikiano . . . kana kwamba wakati wako hauna maana yo yote . . . . Ndege zinapeleka maelfu ya mifuko kusikofaa.”
Kati ya mifano mingine inayoweza kutajwa ni kushindwa kwa wenzi wa ndoa kuchukua wajibu wao kwa uzito. Hata lililoenea sana, watu kwa jumla hawajali kabisa wajibu wao kumwelekea Muumba wao, Yehova Mungu.—Ayubu 35:10, 11.
Kuna sababu mbalimbali kwa wengi namna hiyo kushindwa kuchukua wajibu wao kwa uzito. Kwa mfano, inapokuja kwa upande wa Mungu, jibu la wazi ni, kwa sababu ya kukosa imani. Nia ya wengi ni kwamba Mungu amefariki, au Mungu haoni au hajali, au Mungu hatafanya lo lote juu yake.—Eze. 8:12; 2 The. 3:2.
Inapokuja kwa wajibu mwingine, wengi wanajaribu kueleza kulingana na akili zao wenyewe. Wanaeleza kushindwa kwao kulipa kodi juu ya msingi wa kwamba sheria za kodi ya mapato mara nyingi zinawapendelea matajiri, au kwa sababu fedha ya kodi inalipwa kwa wakulima matajiri kwa kutokuza mavuno. Anapokuwa na ugumu wa kupata uchumi, baba anaweza kuona kwamba kupunja kwa habari ya kodi si jambo kubwa sana. Halafu tena, mume anayejifanya kumpenda mkewe huenda akatoa sababu ya udanganyifu wake wa wajibu kwa mkewe juu ya msingi wa kwamba mkewe ni mvivu au haoni ubora wa mumewe.
Sababu gani tunapaswa kuchukua wajibu wetu kumwelekea Mungu na mwenzetu kwa uzito? Kwanza, kwa sababu Mungu yuko. Ulimwengu wote uu huu ni ushuhuda wa kuwako kwake. Anaona yote; “hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.” Na kama Neno lake lituonyavyo: “Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.”—Ebr. 4:13; 1 Tim. 5:24.
Inatupasa tuchukue wajibu wetu kwa uzito kwa sababu ndilo jambo la haki, linalofaa kufanywa. Hatuwezi kuepuka maana ya kanuni ya kumtendea mwenzetu kama tunavyotaka yeye atutendee. Ili kuwa na dhamiri safi, ili kujiheshimu, inatupasa tujitahidi kwa unyofu wa moyo kuishi kulingana na tunayojua ni haki. Kuna uradhi, kuna kujisikia wenye nguvu tunaposhinda jaribu kuidanganya serikali, au wenzi wetu au jirani yetu. Anayeishi kulingana na wajibu wake ni shujaa kama simba, lakini anayeshindwa kufanya hivyo ni kama fisi mwenye kujifichaficha.—Mit. 28:1.
Na zaidi, kila mara kuna maelekeo ya kugunduliwa. Inapokuwa hivyo kunaweza kuwa na faini na hata kifungo pamoja na kuaibishwa. Woga wa matokeo kama hayo unapaswa uwe kama kizuio.
Zaidi wazazi wana daraka katika jambo hili, la kutia ndani ya watoto wao kabisa takwa la kuchukua wajibu kwa uzito na kuzoea lile lile wao wenyewe. Hata mbele ya umri wa kwenda shuleni, watoto wanaweza kufundishwa kukubali kutunza matakwa yao wenyewe na kuzoea tabia ya kuwa wenye utaratibu, kama vile kuondoa vitu vyao vya kuchezea.
Wanapokua zaidi wanaweza kufunzwa kuwafanyia wengine mambo, kuwasaidia ndugu zao wachanga na dada, kumsaidia mama katika kazi yake ya nyumbani au baba katika kazi zinazompasa kufanya nyumbani. Wanapaswa kufunzwa kuwa watu wa kutegemewa, kumaliza wanachoahidi au kukubali kufanya. Wanapaswa vile vile kufundishwa kukubali wajibu wa matendo yao. Wanapaswa kufundishwa kukubali matokeo ya makosa yao wenyewe na si kujaribu kujitungia udhuru au kuwalaumu wengine. Mafundisho hayo yote yatawasaidia kuchukua wajibu wao kwa uzito wanapoanza kujitegemea wenyewe.
Bila shaka lo lote, wanaopaswa kushughulikia zaidi kuliko wengine wote kuchukua wajibu wao kwa uzito ni watumishi walioweka wakf wa Kikristo. Wakiwa walichukua wajibu wenyewe wa kufanya mapenzi ya Mungu, zaidi wana daraka kwake Yeye. Wana wajibu wa kulipa vitu vya Kaisari kwa Kaisari lakini vitu vya Mungu kwa Mungu. (Marko 12:17) Linalotiwa ndani katika kulipa vitu vya Kaisari ni kodi. Kulipa vitu vya Mungu kwa Mungu kunatia ndani na kuchukua kwa uzito agizo lao la kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu na ufalme. (Isa. 43:10-12; Mt. 24:14) Inatia ndani vile vile na kuchukua kwa uzito wajibu wao kuishi maisha mema, safi, ya Kikristo. Na inatia ndani kuchukua kwa uzito wajibu wao kukusanyika pamoja na Wakristo wenzao kwa kusudi la kutiana moyo wao kwa wao.—Gal. 5:22, 23; Ebr. 10:24, 25.
Sababu gani kuchukua wajibu kwa uzito? Kwa ufupi, kwa kuwa Mungu anataka hivyo. Kwa sababu ndilo jambo linalofaa, la hekima, ndiyo, la kuthawabisha zaidi.