Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w75 1/15 uku. 47
  • Imara kwa Utawala wa Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imara kwa Utawala wa Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
w75 1/15 uku. 47

Imara kwa Utawala wa Mungu

“MASHAHIDI WA YEHOVA WAENDA NYUMBANI”​—hiki ni kimojawapo cha vichwa kadha vinavyofanana vilivyoandikwa katika kurasa za kwanza za magazeti makubwa ya kila siku katika Netherlands Julai 31, 1974. Ni nini kilichotukia kufanya habari hizi ziandikwe?

Siku hiyo magazeti yalitaja upeo wa mfululizo wa hatua ambazo Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Hukumu ilichukua katika Netherlands juu ya mashahidi wa Yehova wa Kikristo waliokuwa wametimiza umri wa kuweza kuingia jeshini. Ugumu ulikuwa kwamba vijana wenye adabu njema, ambao “uhalifu” wao wa pekee ulikuwa kukataa wasizoezwe kuua wengine, walitiwa gerezani kando ya wahalifu washupavu, nyakati nyingine kwa vifungo virefu zaidi kuliko walivyopata wahalifu hao. Mashahidi hao vijana wa Yehova walifuata hali hii kwa sababu waliutambua utawala wa Mungu kama wenye haki ya kwanza katika maisha zao.

Miaka kadha iliyopita hatua ya kwanza katika mifululizo hii ya matendo ilichukuliwa na Wizara ya Hukumu. Hii ilifanya mashahidi wa Kikristo wa Yehova wapewe ruhusa ya kuwa na vitabu vinavyofundisha Biblia gerezani. Baadaye Mashahidi walipelekwa sehemu nyingine ya gereza, walikoishi chini ya hali zisizo na magumu sana. Hata waliruhusiwa kuwa na makusanyiko yao wenyewe, na wajumbe wa afisi ya tawi ya Watch Tower Society katika Amsterdam waliruhusiwa kuwatembelea na kutoa hotuba. Baadaye tena, hawa Mashahidi vijana waliruhusiwa kuondoka gerezani wakahudhurie makusanyiko ya kitaifa na ya mataifa yote ya mashahidi wa Yehova. Hata waliruhusiwa kwenda nyumbani juma nyingine.

Zaidi ya hayo, maafisa wa Wizara ya Ulinzi walikuwa na mazungumzo mengi na wajumbe wa Watch Tower Society. Julai 11, 1974, Wizara ya Ulinzi iliwatangazia wajumbe hawa wa Sosaiti kwamba Mashahidi waliobatizwa wasingelazimishwa kuingia katika utumishi wa jeshi tena.

Wizara ya Hukumu ndipo ilipojitokeza tena. Ikaamuliwa kwamba kwa kuwa Wizara ya Ulinzi inafanya kazi kulingana na sheria ya wazi katika shauri hili, haikuwa lazima tena kwa Mashahidi waliokuwa gerezani tayari kuendelea kukaa humo. Kwa hiyo Mashahidi hawa wote wakafunguliwa.

Gazeti Nieuwsblad van het Noorden la Julai 31, 1974 lilisema hivi: “Sheria inatungwa kumpa kila Shahidi wa Yehova aliyebatizwa ruhusa ya kutoingia katika utumishi wa jeshi. Kwa kuahirisha mazungumzo ya sheria hii iliyotolewa na maneno ya watu hatua zote juu ya [mashahidi] wa Yehova zimekomeshwa.”

Hivyo kwa sasa Mashahidi vijana waliobatizwa katika Netherlands hawana wajibu wa kufanya kazi ya jeshi. Wanashukuru kwa hatua ambayo maafisa wa Holland wamechukua kwa ajili yao. Bila shaka maafisa wa serikali waliujua unyofu wa vijana hawa waliokata shauri la kuwa imara kwa ajili ya utawala wa Mungu kwa sababu ya wakf wao kwa Yehova, Yeye wanayemtambua kama mwenye haki ya kwanza katika maisha zao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki