Kujizuia kwa Wanawake Wasiingiliwe
● Baada ya kuchunguza visa 36 vya wanawake waliokuwa karibu kuingiliwa, na vingine 36 vya wanawake walioingiliwa hasa, Frank J. Javorek wa Denver General Hospital alitaja sababu kubwa zilizofanya wengine waingiliwe kabisa na wengine wasiingiliwe. Kulingana na gazeti “Science News,” mambo makubwa yaliyofanya wengine waingiliwe na wengine wasiingiliwe ni “kama mwenye kuingiliwa alipiga makelele au akapaza sauti kuomba msaada, na kama alijaribu kukimbia. Jambo jingine la maana zaidi ni jinsi mtaa anamoishi mtu huyo ulivyo na kama yeye alikuwa macho kabisa wakati aliposhambuliwa.”
Bila shaka, katika hali fulani mtu hasikiwi anapopiga makelele, tena inakuwa haiwezekani kukimbia. Lakini, wanawake 86 kwa 100 waliopiga makelele, na kukimbia pia, hawakuingiliwa.
Linalopendeza ni kwamba, sheria ya Mungu kwa Waisraeli wa kale ilisema wazi kwamba, ikiwa msichana aliyeposwa alifanya uasherati na mwanamume, wote wawili walipaswa kuuawa. Lakini, ikiwa msichana alipiga makelele kuomba msaada, lakini kusiwe na mtu wa kumsaidia, alionekana hana hatia kwa sababu ya makelele yake. Basi mwanamume peke yake ndiye aliyeuawa, naye msichana akaachiliwa.—Kum. 22:23-27.