Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 8/1 uku. 24
  • Je! Wakumbuka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wakumbuka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Tunaweza Kuwa na Uhakika Ulimwengu Bora Umekaribia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 8/1 uku. 24

Je! Wakumbuka?

Umesoma matoleo ya karibuni ya Mnara wa Mlinzi kwa uangalifu? Ikiwa ndivyo, bila shaka utayakumbuka mambo haya:

● Ni mambo gani yanayoeleza kwa sababu gani ufalme wa Mungu haujachukua uongozi juu ya mambo yote ya dunia?

Yehova Mungu hatawali kwa kutumia nguvu tu. Yeye anataka raia wanaomtii kwa moyo wa kupenda ambao wameelimishwa wamjue. Kuwaelimisha namna hiyo kunachukua muda, vilevile wakati ulihitajiwa wa kuchagua na kuelimisha jamii itakayotawala. Zaidi ya hayo, limekuwa kusudi la Mungu kutoa msingi imara wa kuwa na imani katika utawala wake, kufunua kanuni za serikali yake, kuonyesha sifa zake kama Mtawala wa ulimwengu wote na kutoa kitambulisho kilicho wazi cha kumtambulisha Masihi, Mfalme ambaye angetawala katika jina lake.​—⁠6/15 uku. 13, 14.

● Ni kwa sababu gani nabii Yeremia aliamriwa asioe?

Hii ilionyesha kwamba neno la Yehova kuhusu kuangamizwa kwa Yerusalemu lingetimia bila shaka. Kwa njia hiyo nabii huyu asingezaa watoto wa uharibifu. Kwa sababu Yeremia alijitia sana katika kazi yake ya kinabii yeye alitii amri ya Yehova bila kulalamika.​—⁠6/1 uku. 14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki