Mtumishi Mwaminifu Aiendea Zawadi Yake
Ndugu Franz Zürcher alizaliwa Novemba 25,1891, akabatizwa Novemba 18, 1918, akaingia utumishi wa Betheli katika Switzerland Juni 15, 1923. Kwa muda wa karibu miaka 55 alifanya kazi kwa uaminifu katika afisi ya tawi ya Watch Tower Society, akatumikia akiwa mwangalizi wa tawi kwa miaka kadha. Ndugu Zürcher alimaliza mwendo wake wa kidunia Mei 13, 1978, baada ya kuugua kwa miezi kadha. Alikuwa amejulikana na kupendwa sana na Mashahidi wa Yehova wengi katika Ulaya na mahali kwingine, nao wote wanafurahia utumishi wake wa uaminifu, na ya kwamba sasa amekwisha pokea zawadi yake.—Ufu. 14:13.