Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w79 2/15 uku. 24
  • Shukrani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Shukrani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
w79 2/15 uku. 24

Shukrani

“Hii ni barua fupi tu ya kuwajulisha namna ninavyothamini makala (tungo) za karibuni katika Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Sana sana makala zilizokuwamo katika Mnara wa Mlinzi wa Septemba 1, 1978, ‘Serikali Yetu ya Ulimwengu Wote Inayokuja​—⁠Ufalme wa Mungu,’ zathaminiwa sana, nazo zapaswa zisaidie watu wote wa Mungu kuona waziwazi majira na nyakati ambazo katika hizo twaishi. Nilipojiweka wakf nimtumikie Yehova katika mwaka 1923 niliazimia kwamba nitakuwa nikisoma kila makala katika kila toleo la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Kwa zaidi ya miaka 55 nimetimiza azimio hilo kwa uaminifu nami nimesoma kila makala katika magazeti yote mawili. Kufanya hivyo hakujapata kuwa mzigo bali kumekuwa chanzo cha kupatia furaha tele, faraja na elimu. Nawashukuru sana kwa uchunguzi mwingi sana, kujifunza na kazi nyingi mnayofanya kututayarishia Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Tunafaidika kweli kweli kwa chakula hiki cha kiroho.”

​—Kutoka kwa Msomaji wa Muda Mrefu

Asanteni! Asanteni! Asanteni! Sababu gani? Kwa sababu ya makala ya hivi karibuni ya Mnara wa Mlinzi ‘Jambo Jipya Juu ya Jina la Mungu.’ Mimi ni Myahudi walakini sijapata kusikia jina hilo hata kidogo. Hata nilipokuwa nikihudhuria vikundi vya Wayahudi vyenye kufundisha dini sikulisikia hata kidogo. ‘Jina’ peke yake nililosikia ni Adonay (Bwana). Huwezi kuwaza namna nilivyofurahi kusoma ushuhuda huu usioweza kukanushwa katika makala hii ya karibuni zaidi. Natamani sana kupata nakala zaidi. Jambo linalonichukiza zaidi ni kuona jina la Mungu likitukanwa, likitumiwa vibaya na kukosa kulitumia. Makala hii itanisaidia kutimiza tamaa kubwa ya moyo wangu, kulijulisha jina la Muumba wetu wa ajabu. Asanteni! na Yehova awabariki.”

​—Kutoka kwa Msomaji Myahudi

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki