Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 10/1 uku. 24
  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Vichwa vidogo
  • Hekima Haithaminiwi Sikuzote
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 10/1 uku. 24

Mwenye Hekima Alikuwa na Maana Gani?

Hekima Haithaminiwi Sikuzote

Katika ulimwengu huu, mara nyingi mambo hutukia namna ambavyo mtu hangetazamia. Sawa kama Mfalme Sulemani alivyoona: ‘Huenda mwenye hekima akakosa chakula nao wenye maarifa huenda wakakosa kibali.’ (Mhu. 9:11) Sababu ya msingi ya hili ni kwamba mara nyingi wanadamu wanaamua mambo kwa kutazama sura mahali pa namna hali ilivyo hasa.

Mfalme Sulemani mwenye hekima alitoa mfano wenye kutokeza wa jambo hili, lililokuwa “kubwa” kwake. Tunasoma hivi: “Pia nimeona hekima chini ya jua, nayo ni kama hivi, tena kwangu mimi ilionekana kuwa neno kubwa [‘lilinivutia sana,’ New Berkeley Version]. Palikuwa na mji mdogo [mahali padogo sana], na watu ndani yake walikuwa wachache [hivyo, ukiwa na jeshi dogo la kuukinga]; akaja mfalme mkuu juu yake, akauhusuru, akajenga ngome kubwa ili kuupiga. Basi, kulionekana humo mtu maskini mwenye hekima, naye kwa hekima yake akauokoa mji ule; lakini hata hivyo hapakuwa na mtu ye yote aliyemkumbuka yule mtu maskini.” (Mhu. 9:13-15) Isipokuwa mtu huyo maskini alisaidia, mji huo ungeanguka mikononi mwa huyo “mfalme mkuu.” Kama ilivyokuwa, hekima ya mtu huyo maskini ilishinda ngome pamoja na watu wa vita wa mfalme huyo. Hata hivyo, mahali pa watu hao kumshukuru huyo mtu maskini, walimsahau kabisa baada ya hatari kupita.

Sulemani alifikia uamuzi huu kutokana na hilo: “Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi.” (Mhu. 9:16) Ndiyo, mtu asipokuwa na cheo maneno yake hudharauliwa. Hayashikwi kwa uzito. Mara nyingine kwa kukata tamaa, maneno yenye hekima ya mtu maskini yanafuatwa, walakini hatari ipitapo yeye haheshimiwi.​—Linganisha 1 Wakorintho 1:26, 27; 2:8-11.

Hata hivyo, hekima ni ya maana na bila shaka si kila wakati inapodharauliwa kwa sababu tu ya chanzo chake kinyenyekevu. Sulemani aliendelea: “Maneno ya wenye hekima yanenwayo taratibu husikiwa, zaidi ya mlio wake atawalaye katikati ya wapumbavu. Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.”​—Mhu. 9:17, 18.

Kama mwenye hekima alivyoonyesha hapa, ni jambo bora na la akili zaidi kuyasikiliza maneno yenye heshima ya mwenye hekima, hata awe mtu wa chini namna gani, kuliko kuyasikiliza makelele ya mtawala mwenye kuungwa mkono na raia ambao, katika njia na vitendo vyao wanajionyesha kwamba wana maoni ya kipumbavu ya maisha. Kama inavyoonyeshwa katika habari ya yule mtu maskini, faida kubwa sana inaweza kutokana na hekima kuliko vifaa vya vita. Walakini, mtenda dhambi mmoja au mtu mpumbavu anaweza kuleta taabu kubwa. Kwa mawazo yake mabaya, labda yakinenwa kwa sauti kuu, au kwa matendo yake mabaya, anaweza kuzuia mipango iliyopangwa vizuri, aharibu sifa njema ya jamii nzima au atumie vibaya nguvu au mali zao. (Linganisha 3 Yohana 9-11.) Kwa kweli, hekima inapaswa kupendelewa hata wakati watu wanaposhindwa kuwathamini wale walio nayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki