Mithali Yenye Hekima
“Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa [Yehova], bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.”—Mit. 15:8.
Maneno haya yaliandikwa wakati ule ibada ya Yehova ilipokuwa ikifanyiwa hekaluni katika Yerusalemu, ambapo dhabihu za wanyama zilitolewa. Mwisraeli angeweza kutumia fedha nyingi kununua fahali (ng’ombe dume) au mwana-kondoo wa dhabihu. Hata hivyo, mithali hii inafunua kwamba, Mungu alipendelea sala ya unyofu wa moyo ambayo haina bei yo yote kutoka kwa mtu mnyofu, kuliko dhabihu ya mnyama kutoka kwa mtenda mabaya. Kwa hiyo kanuni ya kupimia ya Mungu si hasara anayopata mtu katika kufuata dini, bali hali yake ya moyoni na namna ya maisha yake kwa ujumla. Mstari unaofuata unasema hivi: “Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa [Yehova], bali humpenda mtu afuatiaye wema.”—Mit. 15:9.