Uchawi Waachwa
Miaka fulani iliyopita, katika kisiwa cha Ometepe katikati ya Ziwa Nicaragua katika Amerika ya Kati, aliishi msichana mchanga ambaye babaye alikuwa anafanya uchawi na kuponya kwa uchawi. Alikuwa na sifa ya kuponya waliolemaa kwa kuita roho wabaya. Baada ya kifo chake, hata hivyo, bintiye alilemaa na kulazwa kitandani.
Mwanamke huyo alipewa utibabu na mtu ambaye anafanya uchawi, pia. Walakini siku moja mwangalizi Mkristo mwenye kusafiri alitembea kwake nyumbani na kumpa zawadi—nakala ya Biblia ya “New World Translation of the Holy Scriptures.” Kwa kuisoma, mwanamke huyo aliona amri ya Mungu juu ya uchawi, kama ilivyoandikwa katika Kumbukumbu la Torati sura ya 18. Basi akaachana na utibabu aliokuwa akipewa na mchawi.
Shahidi mwingine alifanya ziara ya pili kwa mwanamke huyo na funzo la Biblia la nyumbani likaanzishwa. Mwishowe, aliulizwa kama babaye aliyekufa alikuwa ameacha vitabu au karatasi zo zote zinazohusiana na uchawi wake, naye mwanamke huyo akajibu kwamba vitoto kadha vya meza vilikuwa vimejaa vitu hivyo. Kwa hiyo wakateketeza vitu hivyo. (Matendo 19:18, 19) Vilevile, mwanamke huyo alisihiwa amwombe Yehova msaada. Muda mfupi baadaye, akaanza kutembea tena.