Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 4/1 uku. 23
  • Kifaa kwa Wanafunzi na Waalimu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kifaa kwa Wanafunzi na Waalimu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 4/1 uku. 23

Kifaa kwa Wanafunzi na Waalimu

Kifaa cha Biblia ambacho kimetayarishwa kisaidie sana sana vijana kimechukuliwa kwa wingi sana na wanafunzi hali kadhalika waalimu katika Australia. Kwa mfano, katika barua moja iliyopokewa na afisi ya tawi ya Sosaiti nchini humo, nakala 200 za kitabu “Kupata Faida zote za Ujana Wako” ziliagizwa.

Barua hiyo ilitiwa sahihi na kasisi wa chuo cha Kikatoliki. Wakati nakala hizo zilipopelekwa, ilitajwa kwamba kasisi yule apate kibali kutoka kwa wakubwa wake kabla ya kuwagawia wanafunzi vitabu vile. Jibu lake lilikuwa kwamba jambo hilo halingeleta tatizo lo lote kwa vile ndiye aliyekuwa mwalimu mkuu wa chuo hicho. Kasisi huyo alikuwa ameipata nakala ya kitabu “Ujana” kwa mara ya kwanza alipokuwa akiwatembelea wagonjwa katika hospitali moja. Alikuwa amefikia kitanda cha mhubiri mmoja wa Ufalme kijana ambaye alitumia vema nafasi hiyo kumtolea kasisi huyo ushuhuda.

Katika mji mmoja wa Australia, Wakristo wanne Mashahidi wa Yehova waliandika shule 20 za ujamii wote, za watu binafsi na za kidini katika eneo lao. Wanawake hao walimfikia mwalimu mkuu kwanza na kumtolea nakala ya kitabu cha “Ujana” kiwe cha maktaba ya shule. Hakuna kilichokataliwa. Mwalimu mmoja alijipatia nakala 20 za kutumia wakati wa mafunzo ya vikundi vikundi. Walipokuwa wakizitembelea shule za kwanza 10, wahubiri hao wa Ufalme waliangusha zaidi ya nakala 300 za kitabu cha “Ujana Wako.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki