Mithali ya Hekima
“Wenye hekima wataurithi utukufu, bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.”—Mit. 3:35.
Mara nyingi mtu anayeonyesha hekima ya kweli anapata utukufu ambao hakuwa anatafuta. Utukufu huo ambao hakuwa anatafuta anaupata kwa sababu watu wengine wanaweza kuona kwamba matendo yake yanalingana na maarifa na ufahamu, kwamba yeye ni mtu aliye mfano bora. (Mit. 12:8; 22:29) Hiyo ni kwa sababu anatafuta kushikamana na hekima ya kimungu. (Yak. 3:13, 17) “Wapumbavu” ni tofauti sana! Wanaweka maanani zaidi vitu visivyoleta utukufu wa kweli wenye kuendelea bali ambavyo baadaye vitawatokezea kukosa utukufu. Kwa sababu ya upumbavu, hawatangulii kuona matokeo yatakuwa nini. Tofauti ni kubwa kama nini kati ya ‘mwenye hekima’ na ‘mpumbavu’!