Zinaweza Kuufikia Moyo Kweli Kweli
Nyimbo za muziki mtamu zinaweza kufanya hivyo. Tena ni jambo zuri kama nini wakati muziki unaofikia moyo unapouchochea moyo huo kwa njia inayofaa. Mama mmoja aliandika maneno yanayofuata kuhusu muziki mtamu unaoitwa “Kingdom Melodies” ambao umetiwa katika tepe za kaseti:
“Nilipofungulia utepe, watoto wangu watatu waliingia katika chumba wasikilize. Kwa ghafula nikatambua kwamba sisi sote tulikuwa tumeacha kufanya tulilokuwa tukifanya, na watoto walikuwa wameanza kuchukua vitabu vyao vya nyimbo. Hata msichana wangu wa miaka miwili aliketi mbele ya chombo chenye kutoa muziki ili aimbe! Tuliimba kila wimbo hata ikawa vigumu kuondoka katika chumba hicho mpaka tulipomaliza kusikia muziki wote. Nyimbo hizo (ambazo zimetayarishwa kwa njia ya kupendeza sana) zikiwa na habari kuhusu Yehova zinaweza kuufikia moyo kweli kweli.”
Hata wewe unaweza kufurahia nyimbo hizo zilizopangwa kwa namna ya muziki mtamu. Kaseti hizi tatu za “Kingdom Melodies 1,” “Kingdom Melodies 2” na “Kingdom Melodies 3,” zinagharimu Kshs. 27/- (Tshs. 45/-) kila moja, na kila moja inaendelea kutoa muziki muda wa karibu saa moja kabla ya kufikia mwisho. Zipokee kaseti zilizoonyeshwa hapa chini kwa kujaza hati yenye anwani iliyopo na kuituma.
Tafadhalini mnipelekee kaseti ambayo (ambazo) nimetia alama. Mtanilipia malipo ya kuzipeleka kwa njia ya posta. Mimi nimewapelekea Kshs. 27/- (Tshs. 45/-).
KINGDOM MELODIES 1 □ 2 □ 3 □