Maoni Bora Zaidi Yenye Mafaa kwa Ndoa ya Kisasa
“Hakika unapaswa kununua magazeti haya uyasome,” ndivyo jirani alivyokatiza maongezi. “Unajua kwa nini nataka mwanamke huyu ayasome?” jirani akamuuliza mwanamke aliyekuwa akimtolea yule mwingine magazeti. “Shukrani kwa vichapo vyenu, nimemrudia mume wangu. Nilikuwa nimemwacha kisha nikakaa na mama yangu muda wa mwaka mmoja na nusu. Mmoja wa watu wenu alikuja akaniachia kichapo kimoja, nikakisoma baadaye. Kilinifanya niamue kumrudia mume wangu. Mimi naendelea kusoma vichapo vyenu na sasa ndoa yangu ni yenye furaha.” Kwa kupewa pendekezo hilo, mwenye nyumba aliyakubali magazeti kwa utayari.
Magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! yanakuwa kwa ukawaida na maoni ya Kibiblia yenye mafaa kuhusu jinsi ya kushughulika na matatizo ya kijamaa. Tupelekee Kshs. 83.00 (Tshs. 240.00), nawe utayapokea magazeti yote mawili (jumla ya nakala tatu kila mwezi) kwa muda wa mwaka mmoja.
Tafadhali mnipelekee uandikishaji wa mwaka kwa magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi nimewapelekea Kshs. 83.00 (Tshs. 240) kwa matoleo 36.