Wewe Unajibu kwa Hasira?
“Jawabu la upole hugeuza hasira; bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.” Ndivyo inavyosema Mithali 15:1.
Wakati unapokasirishwa na mtu fulani, je, unajisikia ukilazimika kumtenda kama alivyokutenda na kutaka ‘kumchemsha kidogo’? Jambo hilo linaweza kuwa na matokeo mazito.
Mjini New York, msichana mdogo alikuja nyumbani baada ya kuhusika katika ubishi mkali kwa sababu hakutumikiwa vizuri katika duka la pizza, naye akamweleza baba yake wa kambo kisa hicho. Baba huyo alienda akaseme na mwenye duka hilo. Ugomvi ukaanza, naye mwenye duka la pizza akampiga risasi na kumuua.
Je, inaweza kuwa kwamba kufuata shauri la mithali iliyotangulia kutajwa kungalisaidia katika hali kama hiyo? Kumbuka kisa kinachohusu Abigaili na Daudi, kama kilivyoandikwa katika 1 Samweli 25:2-35. Daudi alikaribia kufanya kosa zito wakati alipopokea habari mbaya kwa vijana wa kiume waliorudi kutoka kwa Nabali, mumeye Abigaili. Damu isiyo na hatia ingalimwagwa. Jawabu la upole la Abigaili, pamoja na vitendo vyake vya fadhili na unyenyekevu, liliigeuza hasira kali ya Daudi na watu wake.