Mkutano wa Kila Mwaka Oktoba 4,1986
MKUTANO WA KILA MWAKA wa washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania Oktoba 4, 1986, utafanywa katika Jumba la Makusanyiko la Mashahidi wa Yehova, 2932 Kennedy Boulevard, Jersey City, New Jersey Mkutano wa utangulizi wa washiriki peke yao utafanywa saa 3. 30 asubuhi, ukifuatwa na ule mkutano wa ujumla wa kila mwaka saa 4 .00 asubuhi, Jumamosi, Oktoba 4, 1986
Itathaminiwa ikiwa washiriki wa Shirika hilo wataijulisha Afisi ya Mwandishi juu ya badiliko lo lote lililotokea mwaka uliopita katika anwani zao za barua ili barua zile za kawaida za ujulisho na uwakilishaji ziwafikie muda mfupi baada ya Agosti 15
Barua za uwakilishaji, watakazopelekewa washiriki pamoja na ujulisho wa mkutano wa kila mwaka, zinapasa kurudishwa ili ziifikie Afisi ya Mwandishi wa Sosaiti si baada ya Septemba 1. Kama anavyojua kila mshiriki, inampasa ajaze mambo yote yaliyo katika barua ya uwakilishaji na kuirudisha haraka, akitaja kama atakuwapo ama hatakuwapo mkutanoni yeye binafsi. Habari zenye kutajwa katika kila barua ya uwakilishaji zinapasa kusema waziwazi, kwa maana ndizo zitakazotegemewa katika kuamua mapema ni akina nani hasa watakaokuwapo binafsi
Inatazamiwa kwamba kipindi chote, kutia na ule mkutano rasmi wa kishughuli na ripoti, kitamalizwa ifikapo saa 7:00 alasiri au muda mfupi baada ya hapo Hakutakuwa na kipindi cha alasiri. Kwa sababu nafasi ni ndogo, itawezekana kuingia kwa kuwa na tikiti tu Hakutakuwa na mipango ya kuunganisha mahali pengine-pengine kwa kamba za simu ili kuusikia mkutano wa kila mwaka.