Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 8/15 uku. 32
  • Wewe Unasahihishaje Watoto Wako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wewe Unasahihishaje Watoto Wako?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 8/15 uku. 32

Wewe Unasahihishaje Watoto Wako?

HILO si jambo rahisi, labda wazazi walio wengi watakubali hivyo. Wazazi wenye watoto wa umri wa miaka 10 na 7 wanasimulia jinsi vitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu na Kupata Faida Zote za Ujana Wako msaada mkubwa.

“Inapohitajiwa kabisa tusahihishe watoto wetu,” wanaandika, “sisi tunaongea nao na kujaribu kujua ni nini linaloonekana kuwa ndilo tatizo, kwa mfano, labda kutokuonyesha upendo kwa ndugu au dada au kukosa kutuheshimu sisi wazazi. Halafu tunawaambia waende wakasome, wakiwa katika faragha ya chumba chao wenyewe, sura fulani inayofaa kutokana na kimoja cha vitabu hivyo viwili. Pia tunawapa mgawo wa kufungua maandiko fulani wayasome.”

Matokeo yanakuwa nini? “Wanapotokea kutuambia kwamba wamemaliza na wako tayari kurudia kuzungumza sura ile na maandiko yale pamoja na Dadii au Mamii, wanakuwa na badiliko kubwa kama nini!” Kwa habari ya msichana wao wa miaka saba, ambaye ana elekeo la kushikilia sana kauli yake, wao wanaandika hivi: “Ingawa huenda yeye akakimbia kwa kuchukizwa akipita katika upenu wa sebule kuelekea chumbani mwake, anatokea humo akichekelea na kusema, ‘Naweza kuona nilikosea. Pole!’”

Ikiwa wewe ni mzazi au unajua wazazi wanaohitaji msaada katika kuwatia watoto wao nidhamu, mbona usivipate vitabu hivyo visivyo vya bei ghali? Kwa kweli vinaweza kuwa msaada mkubwa katika kulea watoto.

Tafadhali mnipelekee, mkiwa mumelipia malipo ya posta, vile vitabu vyenye jalada gumu vya kurasa 192 vinavyoitwa Kumsikiliza Mwalimu Mkuu na Kupata Faida Zote za Ujana Wako. Mimi nimewapelekea KShs.30.00 (Tshs.80.00).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki