‘Nilisaidiwa kufahamu Mtu niliyedhani singeweza kamwe kumfahamu’
Katika barua ifuatayo kwa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, mtu mmoja anaeleza ni wapi alikopokea msaada huo.
“Mabwana:
“Mimi ningetaka kuwajulisha jinsi vitabu vyenu vinavyonisaidia sana kufahamu Mtu niliyedhani singeweza kamwe kumfahamu. Sasa Biblia ndicho kitabu chenye kuvutia zaidi ambacho nimepata kusoma kwa sababu ya msaada mlionitolea kupitia vitabu vyenu.
“Tafadhali mwaweza kunipelekea orodha ya vitabu vyote mnavyochapisha, ikiwezekana?
“Zilizotiwa ndani hapa ni Kshs. 40/- (Tsh. 110/-; RWF 230) kwa nakala mbili za Reasoning From the Scriptures . . . Ni lazima mimi nishiriki [pamoja na wengine] ‘kisaidizi hiki kidogo’ kilicho bora.”
Tungependa pia kuwezesha kipatikane kwako kitabu hiki cha Biblia cha kusaidia chenye kurasa 448 Reasoning From the Scriptures. Bei yake ni Kshs. 20/- (Tshs.55/-) tu.
Tafadhali tumeni, mkiwa mmelipia gharama ya posta, kile kitabu cha Biblia cha kusaidia, chenye jalada gumu Reasoning From the Scriptures. Ninawapelekea Kshs. 20/- (Tshs.55/-).