Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 6/15 uku. 22
  • Panama Yafurahia Kazi Yayo ya Kujenga

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Panama Yafurahia Kazi Yayo ya Kujenga
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Tatizo la Kujenga
  • Hakuna Mnara wa Babeli
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 6/15 uku. 22

Panama Yafurahia Kazi Yayo ya Kujenga

KUJENGA majengo si jambo jipya katika Panama. Kuelekea mwanzo wa karne hii, kazi ilianza katika mfereji mkubwa unaopita katikati ya shingo nyembamba ya nchi hii, ukiunganisha bahari kuu za Atlantiki na Pasifiki. Kazi hii kubwa sana ya ujenzi iliipa Panama ndogo jina la “njia panda za ulimwengu.”

Katika Januari 18,1986, kazi ya kujenga ya aina nyingine ilifikia upeo wayo. Siku hiyo Mashahidi wa Yehova walifanya programu ya kuzindua makao yao mapya yaliyojengwa ya afisi ya tawi. Ingawa watu 211 peke yao ndio wangeweza kuhudhuria kibinafsi programu ya kuzindua, maelfu zaidi walisikiliza kwa njia ya kuunganishwa kwa simu. Jengo jipya linawapa makao wafanya kazi wa makao makuu, wamisionari, na kiwanda cha kuchapisha.

Hata hivyo, ujenzi wa makao hayo, ni sehemu ya programu ya ujenzi wa kiroho ambao umekuwa ukiendelea katika Panama tangu mwisho wa karne ya 19. Wakati huo mbegu za ukweli wa Ufalme zilipandwa huku. Kufikia mwaka 1957, kulikuwa na zaidi ya wahubiri elfu moja wa “habari njema” katika Panama. (Mathayo 24:14) Afisi ndogo ya tawi na nyumba ya wamisionari iliyojengwa mwaka huo ilitosha. Lakini katika miaka 20 hesabu ya Mashahidi ilikuwa imeongezeka mara tatu! Hivyo katika Septemba 1982 Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova lilitoa kibali afisi ya tawi mpya ijengwe.

Mahali penyewe palikuwa wapi? Kama kilometa 19 nje ya Mji wa Panama mahali pazuri palipokuwa ng’ambo nyingine ya ziwa.

Tatizo la Kujenga

Lakini ni nani ambaye angechora jengo hilo? Lingejengwaje na ni nani angejenga? Tukikumbuka maneno ya Zaburi 127:1, akina ndugu walisonga mbele, wakijua kwamba Yehova angewasaidia wavishinde vipingamizi hivi vilivyoonekana kuwa haviwezi kushindika.

Mchoro wa ramani za kujaribia ulifanywa, ukionyesha kiasi cha nafasi inayohitajiwa kwa afisi, maktaba, mahali pa kuweka akiba ya vichapo, kiwanda kidogo cha kupiga chapa, na makao ya wafanya kazi wa makao makuu. Jumba la Ufalme lenye nafasi kubwa lilitiwa ndani. Wafanya kazi wa utaalamu wa ujenzi wa makao makuu ya Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi katika Brooklyn, New York, walifuatia kwa kuchora jengo ambalo lingetimiza mahitaji haya.

Baadaye ukaja mwito wa ushindani wa kufanya ujenzi wenyewe. Mamia ya Mashahidi wengi wa mahali hapo walijitolea. Akina ndugu katika United States pia walitoa ustadi na utumishi wao. Katika kipindi cha majuma sita tu, jumla ya wasaidizi 230 walikuwa wamewasili, kutia na wengine kutoka nchi nyingine za Amerika ya Kati.

Akina ndugu wa mahali hapo walikuwa na furaha ya kuzitoa nyumba zao. Hata jamaa moja ilihamia kwenye hema kwa muda ili iwape wenye kujitolea 11 mahali pa kulala. Wengine ambao walikuwa na magari madogo ya shule waliyatoa ili yawasafirishe wafanya kazi hao. Hata hivyo wengine walishiriki katika kutoa vyakula vya bure 30,000 ambavyo viliandaliwa mahali papo hapo pa ujenzi. Vinywaji vyenye kuburudisha vilitengenezwa kutoka mananasi, machungwa, papaya, na maembe, vilevile madafu, yaliandaliwa mara kwa mara ili kuzima kiu cha wale ambao walikuwa wakifanya kazi ngumu katika jua la kitropiki.

Hakuna Mnara wa Babeli

Kazi hiyo iliendelea upesi sana. Katika muda wa majuma mawili kuta zote zilikuwa zimeinuliwa kufika orofa ya pili, vyuma vingine vilikuwa vimewekwa mahali pazo, na sakafu ya Jumba la Ufalme katika orofa ya pili ilikuwa imewekwa. Kazi ya kuweka mabomba ya maji na umeme iliendelea wakati ule ule pamoja na kazi ya ujenzi wa matofali, kupiga lipu, na kuweka madirisha na milango. Katika muda usiozidi mwezi mmoja paa ilikuwa imewekwa, kwa wakati uliofaa ili kutoa ulinzi kutokana na mvua kubwa​—ambayo si ya kawaida wakati huo wa mwaka.

Kulikuwa na matatizo fulani. Nyakati nyingine, wenye kujitolea 800 walikuwapo, na utaratibu mkubwa wa kitengenezo ulihitajiwa ili kuwapa wote kazi ya kutosha. Zaidi, ndugu wengi wageni hawakujua Kihispania. Badala ya jambo hili kusababisha kazi ya kujenga ikome, kama ilivyokuwa katika Mnara wa Babeli wenye sifa mbaya, akina ndugu walionyesha tunda la roho​—nao wakapata usaidizi wa wakalimani.​—Wagalatia 5:22, 23.

Wakati wote wa ujenzi, huo mambo ya kiroho yalitiliwa mkazo. Mikutano ya kundi ya kawaida ilifanyiwa mahali pa ujenzi, na wakati uliwekwa kando wa kushiriki katika huduma ya shambani. Kulikuwako pia na vipindi vya tafrija, kutembelea sehemu zenye kupendeza, na vikusanyiko vya kirafiki. Lakini kwa msingi akina ndugu walikuwa hapo ili kufanya kazi, na muda si muda majengo yalimalizika!

Katika hotuba yake ya kuzindua, John Booth wa Baraza Linaloongoza alitoa muhtasari wa mambo yote katika njia nzuri, akisema: “Ni jambo gani litatoka katika ujenzi wote huu ambao tumekuwa tukijenga? Kwani, tunajenga kwa umilele wa wakati ujao. Si kwamba ujenzi huu utadumu milele, lakini matokeo ya ujenzi huu na kazi ya akina ndugu nchini pote na ulimwenguni pote yatakuwa watu ambao wataishi milele.” Si ajabu kwamba Mashahidi katika Panama wanafurahia kazi yao ya ujenzi ambayo daima itaendelea!

[Ramani katika ukurasa wa 22]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Panama

Panama City

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki