“Ile Kazi ya Kuchosha Imekwisha Milele!”
Ndivyo alivyoeleza mtumiaji mmoja wa Watch Tower Publications Index 1930-1985 (Kiingereza). Yeye anaongeza: “Funzo la kibinafsi ni tofauti kama nini. . . . Inashangaza jinsi ninavyoweza kupata habari nyingi kwa kipindi kifupi tu cha wakati.”
Kitabu hiki kipya kimetoa fahirisi ya kila kichapo kilichotolewa na Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi Biblia na Trakti tangu 1930. Kwa kukitumia pamoja na maktaba yako ya vichapo vya Mnara wa Mlinzi, unaweza kwa urahisi kupata habari unayotafuta hasa juu ya maelfu ya habari kwa maana halisi, kama vile:
◻ la kufanya na kutofanya katika kutoa nidhamu ya kuzoeza mtoto
◻ jinsi ya kutayarishia mahoji ya kuajiriwa kazi
◻ yasiyopasa kutiwa katika sala
◻ daraka la DNA katika kujigawanya kwa chembe
◻ maoni ya Biblia ya kupanga uzazi
◻ siri ya kuwa na mavazi yenye kupendeza
Tafadhali pelekeeni, gharama ya posta ikiwa imelipiwa, Watch Tower Publications Index 1930-1985 (Kiingereza). Mimi nawapelekea Kshs. 115/-. (Tshs. 315/-)