Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 9/15 kur. 21-23
  • Kutoa Ushuhuda Katika Ile Nchi Yenye Lugha 700

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoa Ushuhuda Katika Ile Nchi Yenye Lugha 700
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Mchanganyiko Mkubwa Sana
  • Lugha Nyingine Yaongezwa
  • Mfalme Asikia “Lugha Iliyo Safi”
  • Lugha Mpya kwa Mwanasiasa
  • Kungali Kuna Ufunzaji Mwingi wa Kufanya
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 9/15 kur. 21-23

Kutoa Ushuhuda Katika Ile Nchi Yenye Lugha 700

JE! WEWE unajua nchi fulani yenye eneo la bara lililo dogo kuliko lile la Hispania, lakini ambayo idadi yao ya watu iko chini sana ya milioni nne wanasema karibu robo moja ya lugha zilizopo ulimwenguni? Je! wewe unaweza kutaja jina la nchi inayochukua nusu moja hivi ya eneo la kisiwa kilicho cha pili kwa ukubwa katika ulimwengu? Kisiwa hicho ni New Guinea, na nchi ile ni Papua New Guinea, na hesabu ya lugha zinazosemwa na wakaaji wayo ni zaidi ya 700! Mchanganyiko huo wa lugha mbalimbali ulitokeaje?

Mchanganyiko Mkubwa Sana

Papua New Guinea ni nchi-kisiwa iliyo umbali mdogo tu kaskazini mwa Australia na digrii chache tu kusini mwa ikweta. Inafanyizwa na visiwa vya kitropiki karibu 600 vilivyotapakaa umbali wa kilometa 1,600. Hata hivyo, zaidi ya sehemu nne kwa tano za jumla ya eneo la bara ya Papua New Guinea ziko katika kile kisiwa kikubwa sana cha New Guinea, ambacho taifa hilo linakishiriki pamoja na Indonesia, upande wa magharibi.

Wakaaji wa kwanza kabisa wa Papua New Guinea wanasemwa kuwa walihamia kule kutoka Asia kupitia Indonesia. Baadaye Wamelanesia na Wapolinesia walijiunga nao. Watu wa kule wanatofautiana katika rangi ya ngozi kuanzia kahawia isiyoshika sana mpaka weusi tititi na katika kimo wanatofautiana kuanzia wafupi na wazito-wazito mpaka warefu na wembamba. Kwa sababu ya sehemu kubwa zaidi ya eneo la ndani ndani kuwa na miamba-miamba, pamoja na misitu yenye miti mingi sana na milima mirefu, yale makabila mengi yaliishi yakiwa ni kama yametengana kabisa na yakakuza lugha zayo wenyewe. Zilizo nyingi kati ya lugha hizo za Kipapua zina sarufi yenye kutatanisha kabisa. Ndiyo, Papua New Guinea ndiyo nchi ile yenye lugha, si lahaja, zipatazo 700!

Katika 1975 Papua New Guinea ilikuja kuwa taifa lenye kujitegemea ikiwa ndani ya Jumuiya ya Madola ya Uingereza: Hiyo ni demokrasi ya kibunge yenye mtawala Mwingereza aliye kichwa cha taifa lakini waziri mkuu akiwa ni mwenyeji. Ingawa Kiingereza ndiyo lugha rasmi leo, hesabu kubwa za wale walio katika vikundi vile vya lugha 700 wanasema moja ya lugha mbili zinazoongewa kwa wingi sana, Hiri Motu au Pidgin ya New Guinea.

Lugha Nyingine Yaongezwa

Hata hivyo, amini au usiamini, miaka kadhaa iliyopita “lugha” moja ilikuwa ingali inakosekana katika hii nchi yenye lugha 700. Ilikuwa ipi? Ilikuwa ile “lugha iliyo safi”​—ukweli unaohusu Mungu na Ufalme wake. (Sefania 3:9) Lugha mpya hiyo haikuletwa katika Papua New Guinea mpaka miaka ya katikati ya 1930.

Yote hayo yalianza katika 1935 wakati Lightbearer, meli ndogo yenye kuendeshwa kwa mota na kikundi cha Mashahidi wa Yehova, ilipoondoka Australia na hatimaye ikatia nanga katika Port Moresby katika pwani ya kusini-mashariki mwa Papua New Guinea. Hiyo ilikuwa ndiyo mara ya kwanza ya wananchi kusikia mvumo wa ile “lugha iliyo safi”—kuusikia kwa uhalisi ujumbe wa Ufalme wa Mungu kama ulivyotangazwa kupitia vifaa vya sauti katika sitaha ya Lightbearer.

Hata hivyo, haikuwa mpaka 1951 kwamba hii “lugha iliyo safi” ikajulikana vizuri zaidi na kutumiwa. Kuanzia mwaka huo na kuendelea, Mashahidi kutoka Australia, Kanada, United States, Ujeremani, Uingereza, na New Zealand walijitolea kwenda kwenye Eneo la Papua na New Guinea, kama lilivyokuwa likiitwa wakati huo. Baada ya kuwapa ushuhuda Wazungu wa huku, walipata upesi njia na namna ya kuongea na Wapapua wenyeji juu ya Ufalme wa Mungu. Kufanya hivyo kulitia ndani kwenda nyumba kwa nyumba, jambo ambalo lilichukua jitihada ya ziada kwa sababu nyumba fulani-fulani zilijengwa juu ya viguzo virefu juu ya maji au katika nchi kavu.

Bila shaka, ili kuwafunza ile “lugha iliyo safi” watu hao wa lugha nyingi, Mashahidi kutoka ng’ambo walilazimika kujifunza angalau moja ya lugha zile mbili zenye kutumiwa kwa wingi sana, au za kibiashara. Hiyo haikutatua matatizo yao yote kwa sababu hakuna yo yote ya lugha mbili hizo iliyokuwa lugha ya mama ya wakaaji bali ilikuwa ni michanganyiko tu ya lugha mbalimbali iliyowezesha watu wenye kusema lugha tofauti-tofauti wawasiliane. Kwa hiyo mara nyingi kutoa ushuhuda kulitia ndani kuchukua hatua ngumu za kusema na mtu fulani katika moja ya lugha zile za kibiashara kisha kumwacha autafsiri ujumbe kwa manufaa ya wengine waliopo.

Mashahidi walianza pia utumizi wa njia asilia za kufunza, kama vile kuchora picha rahisi-rahisi katika ubao wa kuandikia au kifaa kingine cho chote kilichopatikana. Baada ya muda, vitabu na magazeti ya Kibiblia yalikuja kupatikana katika lugha zile za kibiashara za Hiri Motu na Pidgin ya New Guinea. Ile broshua Furahia Milele Maisha Duniani! katika lugha mbili hizi imekuwa yenye mafaa hasa katika kufunza wanakisiwa ile “lugha iliyo safi.”

Mfalme Asikia “Lugha Iliyo Safi”

Yesu Kristo alisema kwamba wanafunzi wake ‘wangechukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.’ (Marko 13:9) Siku ya Agosti 9, 1984, wamisionari fulani wa Mashahidi wa Yehova katika Kisiwa Manus walipewa nafasi ya kumpa mfalme ushuhuda, ingawa chini ya hali za kufurahisha zaidi. Siku hiyo Mwana-Mfalme Charles, mrithi wa kiti cha ufalme cha Uingereza, alitembelea kisiwa hicho.

Katika mitumbwi yao iliyopambwa-pambwa, washiriki wa kabila la Tita walimsindikiza Mwana-Mfalme Charles kutoka meli yake kuja kwenye ufuo, karibu tu upande mwingine wa barabara kutoka nyumba ya wamisionari. Baada ya kukaribishwa na wacheza-ngoma mia moja na kuvikwa taji kuwa “jumbe,” alihudhuria chakula cha mchana, ambacho kwa hicho Waziri Mkuu wa Kisiwa Manus alikuwa amewaalika wamisionari hao. Wakati Mwana-Mfalme alipowauliza walilokuwa wakifanya kisiwani, kwa furaha walimweleza kifupi juu ya kazi yao. Walipendezwa sana kuwa na nafasi ya kumpasha habari kwamba Yehova Mungu ana Mashahidi pia katika Kisiwa Manus kilicho mbali sana.

Kufuatia hilo, afisa wa kike aliyejulisha wamisionari kwa Mwana-Mfalme Charles mwenyewe amekisoma kitabu Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Pindi kwa pindi, mwanamke huyo amepitia kwenye nyumba ya wamisionari kuongea wakati wa kunywa kahawa na kula keki pamoja.

Lugha Mpya kwa Mwanasiasa

Mfanya biashara mmoja wa New Guinea alihusika katika siasa na katika kanisa la Kilutheri. Hata hivyo, kanisa la kwao alilohudhuria lilikuwa limegawanyika sana hivi kwamba mapasta wale wawili wenye kupingana walifanyiza mbari mbili zilizopigana kwa karibu mwaka mmoja zikitumia pinde, mishale, mikuki, na ngao za vita. Pigano hilo lilifanya watu tisa wafe na wengi wakajeruhiwa. Mwanamume huyo aliamua kuliacha Kanisa la Kilutheri lakini hakujua mahali pa kutafuta Wakristo wenye umoja kweli kweli. ‘Hawawezi kuwa ni Mashahidi wa Yehova, kwa maana wao ni manabii wa uwongo,’ yeye akafikiri.

Alikuwa angali na hali hiyo ya akili wakati kikundi cha kwao cha Mashahidi wa Yehova kilipopeleka ombi la kukodi basi yake ili kuhudhuria mkusanyiko wa wilaya. Kwa sababu za kibiashara, yeye alikubali na akaiendesha basi ile yeye mwenyewe. Alihudhuria programu ya Jumapili akavutwa sana na amani na utulivu ulikuwapo, usikivu mwingi sana wa wasikilizaji—watu wazima na watoto—waliofuatana na wasemaji kwa kufungua Biblia zao. Alivutwa hata zaidi wakati wa chakula cha mchana, alipowaona Mashahidi wenye furaha wakipanga mstari kwa subira ili wapate mlo wao, weupe na wasemaji wakingoja zamu yao kama wale wengine na wakila chakula kile kile kimoja. Wakati wa ziara ya kurudi ya muda wa saa sita, aliwasikia Mashahidi wakiimba nyimbo za Ufalme kwa furaha. ‘Jambo hilo lilikuwa tofauti kama nini na Walutheri wenye kupigana!’ yeye akafikiri.

Mwanamume huyo alikubali kujifunza Biblia pamoja na Shahidi wa kwao, lakini kwa siri, asije akaudhi Walutheri wenzake. Hata hivyo, yeye alijipatia nguvu za kiroho kwa haraka ili ajiondoe kanisani na pia kutoka katika utendaji mbalimbali wa kisiasa. Yeye na mke wake walilishiriki “lile badiliko kwenye lugha safi” na wakaanza “kuita juu ya jina la Yehova, ili kumtumikia yeye bega kwa bega” pamoja na mashahidi Wake wenye umoja.—Sefania 3:9, NW.

Kungali Kuna Ufunzaji Mwingi wa Kufanya

Ni kazi nzuri kama nini ambayo inafanywa na wamisionari na Mashahidi wengine ambao wamejitolea kuja kutoka nchi nyinginezo kufunza ile “lugha iliyo safi” katika Papua New Guinea! Kutoka kwa wahubiri wawili tu katika 1951, hesabu ya wahubiri na walimu wa Mashahidi imeongezeka kufikia 1,800, sasa walio wengi kati yao wakiwa wametoka kati ya wenyeji.

Mashahidi hao wenyeji ni chanzo cha kutia moyo wale ambao wametoka nchi nyinginezo kuja kutumikia hapa. Ndugu mmoja Mwingereza anayeishi katika kisiwa cha Bougainville anaandika hivi: “Moja la mambo yenye kutia moyo zaidi yanayotusukuma sisi tuendelee kumtumikia Yehova hapa ni kuona jinsi ndugu zetu wa Papua New Guinea wanavyoendelea kumtumikia Yehova kwa uaminifu, mara nyingi wakiwa chini ya hali ngumu sana. Wengi wao hawana makao yao wenyewe bali wanalazimika kuishi pamoja na watu wa ukoo wao. Mara nyingi wanalazimika kutembea miendo mirefu katika joto jingi au mvua kubwa waje mikutanoni au waende nje katika utumishi wa shambani. Mmoja wa dada zetu wa hapa anaishi kule nje mashambani. Ili aokoe wakati anapokutana nasi kwa ajili ya ushuhuda wa barabarani, mume wake anamvusha mto wakiwa wamekalia mpira mkubwa wa ndani akiwa pamoja na bintiye mdogo na kitoto chake.”

Kungali kuna kazi nyingi ya ufunzaji ya kufanya miongoni mwa wenyeji. Kupendezwa wanapendezwa. Jambo hilo linaonekana wazi kutokana na uhakika wa kwamba watu 10,235 walihudhuria Ukumbusho wa kifo cha Kristo katika 1987. Lakini msaada zaidi unahitajiwa ili kutunza upendezi wote huu katika ile “lugha iliyo safi.” Ni kama vile Shahidi mmoja wa kigeni, aliyekuja hapa kutumikia mahali ambapo uhitaji ni mkubwa zaidi, alivyoeleza: “Moyo wangu unasikitika ninapofikiria watu wengi wanaopendezwa katika vijiji hivi vya mbali mashambani vya Papua New Guinea. Sisi hatuna kabisa wafanya kazi wa kutosha katika shamba hapa. Kwa uhakika kuna uhitaji mkubwa katika sehemu hii ya ulimwengu. Tunajua kwamba Yehova anajua jambo hilo na kwamba yeye atafanya maandalizi ya kuwatunza watu hawa wenye njaa ya ukweli.”

Namna gani wewe? Je! ungependa kushiriki katika kufunza ile “lugha iliyo safi” katika hii nchi yenye lugha 700?

[Ramani katika ukurasa wa 21]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

AUSTRALIA

PAPUA NEW GUINEA

Manus

Port Moresby

Bougainville

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki