Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 11/1 kur. 21-23
  • Uhuru wa Kidini Watetewa Katika India

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uhuru wa Kidini Watetewa Katika India
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Vichwa vidogo
  • Jinsi Swala Hilo Lilivyozuka
  • Watoto Dhidi ya Serikali
  • Tisho kwa Umoja wa Kitaifa?
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 11/1 kur. 21-23

Uhuru wa Kidini Watetewa Katika India

ULE uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi wa Agosti 11, 1986, katika New Delhi uliwashangaza mamilioni. Wakati ambapo utukuzo wa taifa ulikuwa ukipata nguvu, wachache walitazamia kwamba uhuru wa kidini wa kikundi cha wachache ambacho sana sana hakijulikani ungeheshimiwa. Lakini baada ya kuchunguza sana mambo ya hakika, mahakama kuu zaidi ya India iliamuru kwamba watoto wa Mashahidi wa Yehova hawawezi kushurutishwa kuimba wimbo wa taifa. Katika uamuzi wenye kutokeza mahakama hiyo ilisema:

“Sisi tunatosheka, katika kesi iliyopo, kwamba kufukuzwa shuleni kwa wale watoto watatu kwa msingi wa kwamba kwa sababu ya imani yao ya kidini iliyoshikiliwa kwa kudhamiria, wao hawajiungi kuimba wimbo wa taifa katika kusanyiko la asubuhi ingawa wao husimama wima kwa heshima wakati wimbo unapoimbwa, ni uhalifu wa haki zao za msingi ‘kwa uhuru wa dhamiri na kukiri, kuzoea na kueneza dini kwa uhuru.’”

Hakimu 0. Chinnappa Reddy na Hakimu M. M. Dutt wa Mahakama Kuu Zaidi ya India ndio waliokuwa mahakimu waliosikiliza kesi ya wimbo wa taifa ya Mashahidi wa Yehova ambayo sasa inajulikana sana.

Jinsi Swala Hilo Lilivyozuka

Karibu nusu ya Mashahidi wa Yehova 8,000 katika India wanapatikana katika mkoa mdogo wa Kerala katika sehemu ya kusini zaidi sana ya taifa hili kubwa mno. Katika shule zilizo nyingi huko, wimbo wa taifa unaimbwa kila siku. Desturi katika shule hii hasa inayohusika ilikuwa wanafunzi wote waimbe wimbo wa taifa katika korasi. Watoto wa Mashahidi wa Yehova, hata hivyo, walisimama tu huku wengine wakiimba. Kama ulivyosema uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi: “Hakuna mmoja aliyejali. Hakuna mmoja aliyeona wasiwasi. Hakuna mmoja aliyefikiri hilo kuwa utovu wa heshima au utovu wa uzalendo. Watoto waliachwa kwa amani na kwa itikadi zao.” Hiyo ndiyo iliyokuwa hali kwa miaka mingi.

Halafu ukaja Julai 1985. Mshiriki mmoja wa Baraza la Kutunga Sheria la Taifa akapinga kwamba yeye alifikiri ni jambo la utovu wa uzalendo kwa ye yote kukataa kuimba wimbo wa taifa. Jadiliano lilifuata na yale yaliyojadiliwa yalichapishwa katika mengi ya makaratasi ya habari yaliyo mashuhuri katika nchi ile.

Wenye mamlaka wa shule zilizo nyingi katika Kerala, ambao kufikia wakati huo walikuwa wenye kuwahurumia watoto wa Mashahidi wa Yehova, wakawa na woga kwa sababu ya lile pingamizi katika Baraza la Kutunga Sheria na ule utangazaji usiofaa. Kama tokeo, watoto wa Mashahidi wa Yehova walifukuzwa kutoka katika shule moja baada ya nyingine.

Watoto Dhidi ya Serikali

V. J. Emmanuel, ambaye watoto wake wadogo watatu, Bijoe, Binu Mol, na Bindu, walifukuzwa shuleni, alitafuta ponyo la kisheria. Bw. Emmanuel alisadiki kwa uthabiti kwamba sheria ilikuwa upande wake. Yeye alijua kwamba, kulingana na Fungu 25 (1) la Katiba ya India, “watu wote wana haki sawa kwa uhuru wa dhamiri na haki ya kukiri, kuzoea na kueneza dini kwa uhuru.”

Hatimaye Sehemu ya Mahakimu wa Mahakama Kuu ya Kerala ilisikiliza kesi hiyo, lakini ilikataa rufani ya V. J. Emmanuel. Huo ulikuwa mshutuo wenye kushangaza kwa sababu Katiba ya India haisemi kwamba wimbo wa taifa lazima uimbwe ili kuonyesha heshima kwa huo. Inasema tu kwamba inawapasa wananchi “kufuata Katiba na kuheshimu itikadi na sheria zayo, Bendera ya Kitaifa na Wimbo wa Taifa.” Wala hakuna sheria nyingineyo yote inayotaka wananchi wote wa India kuimba wimbo wa taifa.

Rufani ya kesi hiyo ilipelekewa Mahakama Kuu Zaidi ya India. Katika kutangua uamuzi wa Mahakama Kuu ya Kerala, hukumu ya Mahakama Kuu Zaidi ilisema: “Hiyo Mahakama Kuu ilijielekeza vibaya yenyewe na ikapotoka kutoka mwenendo unaofaa. Wao walifikiria, katika mambo madogo-madogo, kila neno na wazo la Wimbo wa Taifa na kukata maneno kwamba hakukuwa na neno au wazo katika Wimbo wa Taifa ambalo lingeweza kuhalifu hisia nyepesi za kidini za ye yote.” Hata hivyo, kama vile Mahakama Kuu Zaidi ilivyotaja kwa usahihi, “Hilo si ndilo swali kabisa.”

Swali ni la kidini, yaani, haki ya watu mmoja mmoja kudumisha uhuru wao wa ibada. Uhakika ni kwamba, Mashahidi wa Yehova hawaimbi wimbo wa taifa wa nchi yo yote. Kwa kweli, nyimbo hizo ni nyimbo za kidini au sala zenye muziki, na Mashahidi wa Yehova wanakataa kwa kudhamiria kuziimba. “Wao wanaacha kuimba kihalisi,” uamuzi wenye ufahamu wa Mahakama Kuu Zaidi ya India ukaeleza, “kwa sababu ya itikadi yao ya unyofu na usadiki kwamba dini yao hairuhusu wao kujiunga na sherehe yo yote isipokuwa iwe katika sala zao kwa Yehova Mungu wao.”

Kwa umaana, Katiba ya India inahakikisha “uhuru wa usemi na elezo,” ambao unatia ndani uhuru wa kukaa kimya. Hilo ndilo jambo ambalo wale watoto walikuwa wakifanya wakati wimbo ulikuwa ukiimbwa wakati wa kusanyiko la asubuhi shuleni—wao walibaki kimya. Hata hivyo, wenye mamlaka ya kielimu huko Kerala walikuwa, kwa kweli, wamepiga marufuku kukimya. Kwa hiyo swali lilizuka kama marufuku hiyo ilipatana na haki zilizohakikishwa na Katiba.

Ile Mahakama Kuu Zaidi ilikata maneno juu ya jambo hili: “Sisi tunaweza kusema kwa mara moja kwamba hakuna uandalizi wa sheria ambao unambidisha ye yote kuimba Wimbo wa Taifa wala sisi hatufikiri kwamba ni jambo lenye utovu wa heshima kwa Wimbo wa Taifa ikiwa mtu ambaye anasimama wima kwa heshima wakati Wimbo wa Taifa unapoimbwa hajiungi katika kuimba.”

Kama ilivyotajwa mwanzoni, wajibu wa kila mwananchi, kulingana na Katiba, ni ‘kuheshimu Wimbo wa Taifa.’ Kwa habari ya heshima kama hiyo, Sheria ya Uzuio wa Kudharau Heshima ya Kitaifa ya 1971 husema: “Ye yote azuiaye kwa makusudi kuimbwa kwa Wimbo wa Taifa au anayesababisha usumbuo kwa kusanyiko lo lote linaloimba hivyo ataadhibiwa kwa kifungo gerezani kwa muda ambao huenda ukafika miaka mitatu, au faini au yote mawili.” Wale watoto wa Mashahidi wa Yehova, hata hivyo, hawakuwa wamepata kamwe kuzuia ye yote asiimbe wimbo wa taifa. Wao hawakuwa wamepata kamwe kusababisha usumbuo kwa kusanyiko lo lote lililokuwa likiimba hivyo.

Tisho kwa Umoja wa Kitaifa?

Mojapo hoja za Serikali ilikuwa kwamba kuimba wimbo wa taifa kulikuwa jambo linalohitajiwa kabisa kwa umoja na ukamilifu wa nchi. Hata hivyo, je! kuimba kwa kulazimishwa wimbo wa taifa kwaweza kweli kweli kuchangia umoja wa nchi au ukamilifu wa wananchi wayo?

Kwa kupendeza, wimbo wa taifa wa India uko katika lugha ya mkoa mmoja tu, na kwa hiyo haufahamiwi na walio wengi wa Wahindi ambao huuimba. Hivyo, kwa walio wengi, kuimba wimbo wa taifa pengine ni jambo lisilokuwa na maana na kwa msingi, linakuwa, sherehe isiyo na maana. Mashahidi wa Yehova hawajiungi katika sherehe kama hizo. Wao wanasali kwa Mungu wao pekee, Yehova.

Pia hoja ilitolewa kwamba ikiwa hukumu ya Mahakama Kuu Zaidi ilipendelea Mashahidi wa Yehova, hilo lingeweza kutisha usalama wa nchi. Lakini Mashahidi wa Yehova katika India ni kikundi cha wachache, chenye hesabu ya watu wapatao 8,000 tu. Je! kikundi kidogo kama hicho kingekuwa tisho kwa taifa la watu zaidi ya milioni 800? Tena, Mashahidi wa Yehova wanajulikana ulimwenguni pote kwa unyofu na utii wao kwa sheria za serikali ambazo chini yazo wao wanaishi.

Katika Naijeria mwanasheria mmoja alisema: ‘Mashahidi ni wananchi walipa-kodi na washika-sheria. Shahidi ye yote ambaye anaweza kuwa mnyofu kwa dini yake kwa kadiri ya kuitii kwa kuhatarisha kupoteza mapendeleo fulani atakuwa mnyofu vivyo hivyo katika mambo mengine yaliyo mengi. Sababu ya kukataa kuiba pesa za serikali hali wafanya kazi wenzi wanaimba wimbo wa taifa na hata hivyo huiba pesa zilizowekwa amana kwao ni kwa sababu Biblia yake ambayo humtaka asiimbe wimbo wa taifa pia inasema haimpasi yeye kuiba.’

Ile sentensi ya mwisho ya hukumu iliyotokeza ya Mahakama Kuu Zaidi yastahili kuangaliwa. Ilisema: “Sisi twataka tu kuongeza: desturi yetu hufundisha uvumiliano, falsafa yetu hufundisha uvumiliano; katiba yetu huzoea uvumiliano; acheni sisi tusiuharibu.” Je! serikali na viongozi watathamini wazo hilo zuri? Je! ule uamuzi wa Mahakama Kuu Zaidi utabaki ukiwa wa mwisho? Ni kupita tu kwa wakati kutaonyesha.

[Picha katika ukurasa wa 23]

Wale watoto watatu ambao kwa heshima walikataa kushiriki katika sherehe za kizalendo

Ile jamaa iliyo wakfu ya wale watoto watatu

Jamaa hii walisoma habari ya kesi hiyo ya mahakama, wakajifunza Biblia, na wakabatizwa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki