Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 11/15 kur. 30-31
  • Kutoka kwa Utumwa wa Kutengeneza Matufali Kwenda Kwenye Uhuru!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Utumwa wa Kutengeneza Matufali Kwenda Kwenye Uhuru!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 11/15 kur. 30-31

Kutoka kwa Utumwa wa Kutengeneza Matufali Kwenda Kwenye Uhuru!

JE! ZILE Piramidi za Giza (karibu na Cairo ya kisasa) zinatukumbusha juu ya watumwa waliotendwa vibaya wakifanya kazi ngumu chini ya jua kali wakikokota mawe makubwa na kuyaweka mahali panapofaa? Na je! unawawazia watumwa Waebrania wakiwa miongoni mwao?

Kwa kweli, zile piramidi za Kimisri zinazoonekana kwenye ukurasa unaofuata ni za zamani za kabla ya wakati ambao jamaa ya baba ya Yusufu Yakobo (au, Israeli) ilipohamia Misri. Lakini ujenzi ulio wa kawaida zaidi ya ule wa kutumia mawe makubwa ni matumizi ya matufali, yanayotengenezwa mamilioni mengi chini ya jua ilo hilo lenye kuwaka vikali.

Waebrania waliokaribishwa katika Misri wakati wa Yusufu walibarikiwa na Mungu kwa ongezeko, wakiwaogopesha sana Wamisri. Tunasoma hivi: “Basi wakaweka wasimamizi juu [ya Waebrania] wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji . . . Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matufali.”—Kutoka 1; 7-14.

Upande wa kulia, unaweza kuona kwamba matufali yangali yakitengenezwa katika Misri, mengine yayo yakikaushwa katika majoko kama lile unaloona hapa. (Linganisha Mwanzo 11:1-3; 19:28.) Hata hivyo, kwa wazi, matufali yaliyo mengi ya Wamisri wa kale yalikaushwa kwa jua. Jambo linaloendelea ni matumizi ya majani makavu katika kutengeneza matufali. Majani makavu yanaonekana katika matufali yanayopatikana katika magofu yaliyochimbuliwa ya Beersheba wa kale (picha ndogo imeonyeshwa).

Kuongeza majani makavu kulifanya matufali yawe yenye nguvu. Ili kuyatengeneza, matope (au udongo), maji, na majani makavu yalikanyagwa-kanyagwa pole pole kwa miguu, kisha yakashindiliwa katika kalibu, na mwishowe yanawekwa nje ili yakauke. Ebu wazia ukifanya kazi ngumu kama hiyo siku moja baada ya nyingine. Kwa kweli, unaweza kufahamu kwa nini Waisraeli ‘waliugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.’​—Kutoka 2:23.

Yehova aliwasikia naye akampeleka Musa kwa Farao ili Waisraeli wapate uhuru. Badala ya hilo, Farao mwenye kiburi aliongeza mzigo wao. Sasa iliwapasa wakusanye majani yao makavu wenyewe na bado watengeneze kiasi kile kile cha matufali kama walivyofanya mmwanzoni. Kwani, huku kulikuwa kama kuhukumiwa kifo! Mungu akasema: “Sasa utaona nitakavyomtenda Farao; maana kwa mkono hodari atawapa ruhusu kwenda zao.”​—Kutoka 5:1–6:1.

Labda wewe unajua ilivyotukia. Yehova alikuwa na uwezo wa kumshinda Farao mwenye udhalimu. Baada ya lile pigo la kumi, Mungu “akawatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri.” (Kutoka 12:37-51) Wakiacha nyuma yale mapiramidi, matufali, na utumwa mkatili, Israeli walipiga miguu kuelekea Nchi ya Ahadi. Mambo kama hayo ya kihistoria yaliyo hakika yanapasa kututumainisha sisi juu ya uwezo wa Yehova Mungu kuandaa uhuru wa kweli kwa Wakristo katika ulimwengu mpya unaokuja, pamoja na dunia Paradiso yao.—Linganisha Warumi 8:20, 21.

[Picha ya ukurasa mzima katika ukurasa wa 31]

[Picha Credit Line katika ukurasa wa 2]

Photos, pages 30, 31: Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki