‘Kilinisaidia Mimi Sana-sana’
Kwa kweli vijana wanahitaji msaada leo, kwa kuenea sana kwa kujiua kwa vijana matineja, mimba, uzoevu wa kileo, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, na matatizo mengine. Lakini wao wanaweza kuupokea wapi? Kijana mmoja kutoka Buffalo, New York, aliandikia Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi:
“Mimi nimekisoma kitabu chenu . . . Kupata Faida Zote za—Ujana Wako. Lazima mimi niseme kwamba ninyi mmeandika kitabu kizuri. Kimenisaidia mimi sana-sana, nami najua kwamba kinaweza kumsaidia mwingine pia. . . . Nimempa rafiki kitabu changu, naye amefanya maendeleo fulani. Asante sana, Bwana, mara milioni moja, kwa kuandika kitabu kama hicho kizuri sana.”
Wewe unaweza kupokea kitabu hiki cha mfukoni chenye thamani cha vijana kwa kujaza na kutupelekea hati iliyopo chini, pamoja na mchango wako.
Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu chenye jalada gumu, chenye kurasa 192 Kupata Faida Zote za—Ujana Wako. Mimi nimewapelekea Kshs. 15/- (Tshs. 45).