Kwa Sababu Gani Uyakose?
Akiwa amesimama katika mstari katika benki moja ya Mjini New York kiangazi kilichopita, mwanamke mmoja wa makamo aliona kwamba mwanamume aliyekuwa mbele yake alikuwa anasoma gazeti Mnara wa Mlinzi. Mwanamke huyo alitaka sana kusoma makala moja iliyokuwamo juu ya sala, kwa hiyo akaandika tarehe ya toleo hilo.
Siku chache baadaye, Mashahidi wa Yehova walitembelea nyumba yake, naye akauliza: “Je! ninyi mna matoleo ya Julai ya Mnara wa Mlinzi?” Baada ya kujua ni kwa sababu gani yeye alipendezwa na gazeti fulani mahususi, mmoja wa Mashahidi alisema hivi: “Njia bora zaidi ya kutokosa lo lote la matoleo yanayopendeza ni kuandikisha.”
“Sikujua mtu angeweza kufanya hivyo!” mwanamke huyo akasema kwa kushangaa. Alipoambiwa andikisho la mwaka ni dola 5, yeye alijibu: “Mna uhakika? Dola 5 tu kwa mwaka mzima?” Alipohakikishiwa ndivyo ilivyokuwa, yeye alitaka si Mnara wa Mlinzi tu bali pia gazeti jenzi lake Amkeni! “Je! mna uhakika ninaweza kupata magazeti yote mawili kwa dola 10 tu?” yeye akauliza tena.
Mwanamke huyo alifurahia kuambia Shahidi huyo amwandikishie. Wewe pia unaweza kupelekewa magazeti Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Peleka Kshs. 97/-tu, na utapokea magazeti yote mawili (nakala tatu kwa mwezi) kwa mwaka mmoja.
Tafadhali mnipelekee andikisho la mwaka mmoja la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Mimi ninawapelekea ninyi Kshs. 97/- (Tshs. 360.00; RWF 600).