Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 4/15 kur. 3-4
  • Wakati Watoto Wanapozaa Watoto

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Watoto Wanapozaa Watoto
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutafuta Matatuzi
  • Wasichana Wanaopata Mimba Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2004
  • Kutoa Mimba—Si Suluhisho Lisilo na Madhara
    Amkeni!—2009
  • Je, Utoaji-Mimba—Ndio Suluhisho?
    Amkeni!—1995
  • Mimba za Utineja—Msichana Apaswa Kufanya Nini?
    Amkeni!—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 4/15 kur. 3-4

Wakati Watoto Wanapozaa Watoto

“MWANAMUME huyo alinizindua sana mpaka ikaonekana kama kwamba jambo hili lilifanyika katika hadithi ya mazimwi tu,” mwanamke kijana tutakayemwita Sharon anakumbuka kwa uchungu. “Yeye alikuwa akiniambia wakati wote kwamba anipenda na kwamba ikiwa msichana rafikiye angepata kuwa na mimba, yeye hangemwacha kamwe.”

Siku moja Sharon alizuru daktari wake akachunguzwe alichokifikiria kuwa maumivu ya kidole-cha-utumbo; kumbe ikawa kwamba alikuwa na mimba ya miezi mitatu. “Mara moja nilimpigia simu mvulana rafiki yangu,” Sharon anakumbuka. Yeye alijibizaje? “Lazima utoe mimba! Kiondolee mbali kitu hicho!” Iliyoonekana kama hadithi ya mazimwi tu ikawa imekuwa jinamizi la usiku.

Wasichana-matineja karibu milioni moja katika United States tu wanapata mimba kila mwaka. United States ina sifa yenye kutilika shaka ya kuwa na kadiri kubwa zaidi ya mimba miongoni mwa bara zilizo na maendeleo ya viwanda—ndiyo bara moja tu ambako kadiri hiyo imeongezeka katika miaka ya majuzi. Hata hivyo, uchunguzi wa nchi 37 uliofanywa na Taasisi ya Alan Guttmacher unafunua kwamba mimba miongoni mwa vijana-matineja wasiofunga ndoa ni tatizo la duniani pote.

Waliandika hivi watafiti Black na DeBlassie katika jarida Adolescence: “Wasichana wa umri wa kwenda shule ambao wanapata mimba wanatoka katika tabaka zote za kijamii na kiuchumi na katika shule za serikali na hata za watu hinafsi. Jamii zote za watu, imani zote, na sehemu zote za nchi, mashambani na mijini, zinawakilishwa.” Kwa habari ya sababu inayofanya kadiri za uzazi ziwe kubwa zaidi miongoni mwa wasichana wa kutoka jamaa za walio maskini au wachache, Journal of Marriage and the Family linasema: “Mara nyingi wasichana wa weupe na wa wenye D[araja] B[ora] K[ijamii na] K[iuchumi] wanatoa mimba.”

Katika United States, wanawake walio chini ya umri wa miaka 20 ndio wanaotoa theluthi moja ya mimba zote zinazotolewa kwa halali. Bila kutia ndani maadili yanayohusika, mara nyingi inakuwa vigumu kuishi kwa kufikiria uamuzi ule wa kutoa mimba. “Acha nikuambie,” akumbuka mwanamke mmoja aliyetoa mimba akiwa angali kijana-tineja tu, “inaumiza kujua kwamba mimi ndiye nilisababisha uuaji fulani, uuaji ambao jeruhi aliyepatwa nao hatakuja kamwe kujua jinsi ninavyosikitika.”

Kutafuta Matatuzi

Kuwa sifa mbaya miongoni mwa watu, ndoa zisizo na uthabiti, umaskini—hayo ni matokeo ya kawaida ya mimba ya utineja. Basi, si ajabu sana kwamba jambo hili limekuwa la kuhangaikiwa na waelimishaji, madaktari, wanasiasa, na wazazi. Watu fulani wanaitisha programu ya elimu ya ngono, hata kudai kwamba vijana wafanyiwe iwe rahisi kupata vizuia-uzazi na kutoa mimba.

Ingawa hivyo, vijana fulani wana mahitaji ya hisia za moyoni ambayo elimu ya ngono haiwezi kutosheleza. Mathalani, wasichana fulani kwa kweli wametaka kupata mimba! Kama kisichana mmoja alivyoeleza jambo hilo: “Mimi nilijaribu kujiingiza matatani ili nivute fikira za wazazi wangu. Nilikadiria kwamba [kitoto] hiki kingekuwa kitu ambacho kingeweza kuwa changu—hakuna mtu angeweza kukichukua, nami nj. ngekuwa na kijipande kilichotokana na mimi ambacho kingenipa sababu ya kuwa hai.”

Zaidi ya hilo, programu za elimu ya ngono haziwapi vijana mwongozo wa kiadili. Bara kama vile Sweden na Uholanzi, ambako programu hizo ni kawaida, huenda zikawa zina mimba chache za utineja lakini ngono za ovyo-ovyo zimeenea sana. Je! ingeweza kuwa kwamba zaidi ya ngono za ovyo-ovyo kuleta mimba, pia zinaleta hasara kubwa za hisia za moyoni, za kiadili, na kiroho? Ikiwa ndivyo, je! kuna sababu zinazofaa za kutia moyo, si utumizi wa vizuia-uzazi, bali usafi wa kiadili? Katika kujibu, acheni tutazame yale ambayo kitabu cha zamani kuliko vyote vilivyoko—Biblia—kinasema juu ya jambo hili.

[Blabu katika ukurasa wa 3]

“Wasichana wa umri wa kwenda shule ambao wanapata mimba wanatoka katika tabaka zote za kijamii na kiuchumi na katika shule za serikali na hata za watu binafsi. Jamii zote za watu, imani zote, na sehemu zote za nchi, mashambani na mijini, zinawakilishwa.”​—Jarida Adoiescence

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki