Mpiganaji Thabiti kwa Ajili ya Ukweli
MARTIN POETZINGER, mshiriki wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova, alimaliza mwendo wake wa kidunia akiwa Mkristo mpakwa-mafuta mapema katika jioni ya Alhamisi, Juni 16, 1988. Yeye alikuwa amekuwa katika afya yenye kuzorota kwa muda fulani lakini alikufa bila maumivu makubwa kule Betheli ya Brooklyn. Mke wake, Gertrud, alikuwa amekuwa kando yake muda wote wa ugonjwa wake.
Ndugu Poetzinger alizaliwa Julai 25, 1904, katika Munich, Ujeremani. Yeye alibatizwa siku ya Oktoba 2, 1928, na akaingia utumishi wa painia siku ya Oktoba 1, 1930. Katika vuli ya 1933, Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi ilimgawia yeye kutunza masilahi za Ufalme katika Bulgaria, lakini katika muda wa mwaka mmoja Mashahidi wasiokuwa wazaliwa wa taifa hilo walihamishwa nchini. Mhamo uliofuata wa Ndugu Poetzinger ulikuwa kwenda Hangari. Alipokamatwa na kuhamishwa kutoka humo nchini kwa njia ya ubandia, ndipo yeye alipopewa uangalizi wa kikundi kimoja cha mapainia katika Yugoslavia. Baada ya ugonjwa mkubwa, uliofanya ahitajiwe kabisa kukaa hospitali muda mrefu katika Zagreb, yeye alirudi Ujeremani.
Ndugu na Dada Poetzinger walifunga ndoa katika 1936, lakini katika mwaka huo huo yeye alipelekwa kwenye kambi ya mateso kwa kukataa kukana imani yake. Mke wake alifungwa gerezani mahali pengine, lakini yeye akapelekwa Dachau halafu kwenye kambi ya uangamizi kule Mauthausen, Austria ya Juu. Huko polisi wa siri walitumia njia ya ugawaji kidogo mno wa chakula, upigaji viboko, na mateso yenye unyama usioelezeka ili kushawishi yeye na Mashahidi wengine kuvunja ukamilifu wao kwa Yehova Mungu. Lakini Ndugu Poetzinger alishika sana imani ya kweli.
Baada ya miaka tisa ya kufungwa gerezani kwa ukatili, Ndugu na Dada Poetzinger waliungamana tena katika 1945. Muda mfupi baada ya hapo, yeye alianza kutumikia katika kazi ya mzunguko katika Ujeremani, na baadaye Gertrud akasafiri pamoja naye, akifanya kazi kwa juhudi katika shamba alipokuwa akitumikia makundi. Katika 1958 yeye alihudhuria Shule ya Biblia ya Gileadi ya Mnara wa Mlinzi, halafu aliporudi Ujeremani, yeye na mke wake wakaendelea katika kazi ya kusafiri mpaka walipoingia utumishi wa Betheli huko katika 1977. Katika Septemba 1977, Ndugu Poetzinger aliwekwa rasmi kwenye Baraza Linaloongoza na akaweza kuja kwenye makao makuu ya Sosaiti katika Brooklyn, New York, baada ya muda unaozidi kidogo mwaka mmoja tangu hapo. Yeye alitumikia pamoja na Halmashauri ya Utumishi ya Baraza Linaloongoza na Halmashauri ya Idara ya Utumishi.
Ndugu Poetzinger alikuwa mpiganaji shujaa kwa ajili ya ukweli. Ushikamanifu wake na utegemezo wa juhudi kwa tengenezo la Yehova na kazi ya Ufalme ulikuwa kielelezo chema kweli kweli. Kwa hiyo sisi tuna uthabiti wa kwamba yeye ni miongoni mwa wale ambao maneno haya yanatumika kwao: “Wenye furaha ni wafu ambao wanakufa katika muungano pamoja na Bwana . . . Ndiyo, roho inasema, . . . mambo ambayo wao walifanya yanaenda moja kwa moja pamoja nao.”—Ufunuo 14:13, NW.
[Picha katika ukurasa wa 31]