Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 10/15 kur. 22-24
  • Cayman Visiwa Vilivyosahaulika Baada ya Muda Kupita

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Cayman Visiwa Vilivyosahaulika Baada ya Muda Kupita
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Vichwa vidogo
  • Kasa, Maharamia, na Tekinolojia ya Hali ya Juu
  • Wageni wa Aina Nyingine
  • Watu wa Cayman Wasikia Zile Habari Njema
  • Upinzani Washindwa Katika Cayman Brac
  • Wakumbukwa na Yehova
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 10/15 kur. 22-24

Cayman Visiwa Vilivyosahaulika Baada ya Muda Kupita

WEWE unaweza kuogelea katika yale maji matulivu ya buluu. Wewe unaweza kupiga mbizi ukapeleleze vyombo vingi vilivyoharibikia kwenye sakafu ya ile bahari kuu. Au unaweza kufanya ziara kwenye shamba lenye kasa. Wapi? Katika Visiwa vya Cayman​—Grand Cayman, Cayman Brac, na Little Cayman.

‘Lakini viko wapi hasa hivyo Visiwa vya Cayman?’ huenda wewe ukauliza. Hilo ni swali lenye kueleweka kwa sababu hivyo ni vidogo sana hivi kwamba ni mara chache sana vinapoonyeshwa katika ramani za ulimwengu. Wakati vinapoonyeshwa, huenda vikaonyeshwa kuwa vijitone vidogo sana tu katika Bahari ya Karibbea ya Magharibi, kilometa 240 kusini mwa Cuba, au kama kilometa 800 kusini mwa Miami, Florida.

Vikiwa vimevumbuliwa katika 1503 na Christopher Columbus katika safari yake ya mwisho baharini kupitia West Indies, visiwa hivyo​—Cayman Brac na Little Cayman, kwa kuwa Columbus hakupata kamwe kuona Grand Cayman​—viliitwa Las Tortugas (Akina Kasa). Hiyo ilikuwa kwa sababu ya hesabu kubwa ya kasa walioonwa wakiwa katika visiwa hivyo na sehemu zenye kuvizunguka. Katika 1670, kupitia Mkataba wa Madrid, Hispania iliipa Uingereza haki ya kuchukua visiwa hivyo, navyo vimebaki vikiwa koloni la Uingereza tangu wakati huo.

Kasa, Maharamia, na Tekinolojia ya Hali ya Juu

Katika siku zile za meli kubaharia-baharia, visiwa hivyo vilikuwa kibandari cha vituo vifupi vya meli kubwa zenye kupita-pita katika maji ya Karibbea. Wale kasa-bahari tele wa rangi ya kijani wakawa chanzo kinachofaa sana cha nyama iliyo mbichi vizuri kwa mabaharia hao wenye njaa. Kasa hao waliliwa wakiwa wabichi-wabichi, au walipelekwa melini wakiwa wamekaushwa au wakiwa wamekaangwa kwa chumvi. Wakawa chanzo kikubwa cha protini wakati wa safari ndefu za baharini.

Lakini visiwa hivyo vilijulikana kwa jambo jingine. Ule utambarare wa ardhi na bandari zilizo salama ni mambo yaliyovutia watu wenginewo wa bahari za maji makuu. Watu wabaya sana wenye meli za kibinafsi na maharamia wa baharini, kama vile Sir Henry Morgan na Edward Teach, aliyejulikana pia kuwa Blackbeard, walitumia visiwa hivyo kuwa maficho yao au vikao vya kuendeshea shughuli zao za kuvizia vyombo vya kibiashara. Kipande hicho cha historia ya kupendeza sana huadhimishwa na sikukuu ya kila mwaka inayoitwa Juma la Maharamia, ambayo huonwa katika sehemu hiyo kuwa jambo kuu la mwakani.

Kadiri ambavyo hesabu ya kasa ilizidi kupungua na meli za stimu zikawa badala ya meli za kuendeshwa kwa matanga, ni meli chache zaidi na zaidi zilizofika mahali hapo. Na kwa kuwa ni wanavisiwa wachache waliokuwa na redio, Visiwa vya Cayman vilikatishwa na kusahaulika na sehemu ile nyingine yote ya ulimwengu kwa makusudi yote yanayofaa. Vikastahili ule mtajo wa kuitwa “Visiwa Vilivyosahaulika Baada ya Muda Kupita.”

Hata hivyo, kufikia miaka ya 1960 hali ilianza kubadilika. Sheria za mahali hapo za ubenki na za kikodi, pamoja na kuja kwa mifumo ya mawasiliano ya tekinolojia ya hali ya juu, ziligeuza eneo hilo lililokuwa limesahauliwa likawa kimoja cha vitovu vya ubenki wa kimataifa ambavyo vinajulikana zaidi. Katika Juni 1987 visiwa hivyo vilihesabu mwaka wavyo wa 500 tangu kufunguliwa benki huko. Badiliko hilo zuri lilihimiza biashara ya utalii. Baraza la utalii la huko lilifurahi sana wakati wageni 8,244 walipozuru katika 1966. Tarakimu hiyo ilikuwa imeruka juu kufikia 430,000 katika 1986, ikifanya biashara ya utalii iwe ya pili kwa umashuhuri kwa kufuatia uundaji wa pesa. Hata hivyo, kuna kikundi kingine cha watu ambao wanapendezwa sana na visiwa hivyo.

Wageni wa Aina Nyingine

Mashahidi wa Yehova, ambao wanachukua kwa uzito maneno ya Yesu kwamba habari njema za Ufalme zitahubiriwa katika mataifa yote, hawakusahau Visiwa vya Cayman. (Mathayo 24:14) Hata kule mapema 1929, Patrick Davidson, aliyekuwa na uangalizi wa kazi ya kuhubiri katika Jameika, alizuru Grand Cayman. Kujapokuwa na upinzani, yeye aliweza kupanda mbegu za ukweli wa Ufalme.

Davidson alifanya ziara ya pili katika 1937, lakini haikuwa mpaka 1950 kwamba shughuli ya kufanya kazi kabisa kabisa katika Grand Cayman ilianzwa na Aleck Bangle na misionari mwenzake. Mamia ya vipande vya fasihi ya Biblia viligawanywa katika muda mfupi. Wamisionari hao waliripoti kwamba waliwapata watu hao kuwa wenye urafiki, walio rahisi kuongea nao, na wenye hamu nyingi ya kusikia zile habari njema.

Watu wa Cayman Wasikia Zile Habari Njema

Wamisionari na wahudumu wengine wa wakati wote waliendelea na kazi yao, kwa uthibitifu na kwa saburi. Kufikia 1959 kulikuwa na kikundi kidogo cha wahubiri wa Ufalme 12, na kundi moja lilipangwa kitengenezo. Mmoja wa wakaaji wa kwanza kule kukubali ukweli wa Biblia alikuwa Wilbert Sterling. Yeye anaweza kukumbuka vizuri siku ambazo kile kikosi kidogo cha Mashahidi kililazimika kufanya kazi katika eneo lao na kulimaliza kwa kupiga miguu. Ingawa sasa yeye ni kipofu na katika miaka yake ya 80, Ndugu Sterling bado anatumikia akiwa mzee katika Kundi la Georgetown.

Jitihada za bidii-endelevu za hao watangazaji wa mapema wa Ufalme zimebarikiwa na Yehova. Sasa kuna wastani wa wahubiri wa Ufalme 60 katikati ya idadi ya watu karibu 17,000. Wengi wa wanavijiji wamekuja kuthamini kwamba Mashahidi ni tofauti kwa sababu ibada yao inategemea msingi wa Biblia.

Mathalani, mwanamke mmoja mwenye kufanya kazi katika mkahawa aliona Shahidi akihubiri nyumba kwa nyumba. Mwanamke huyo akamfikia na kuuliza angelazimika kufanya nini ili awe mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Aliambiwa kwamba angelazimika kutwaa maarifa sahihi juu ya Yehova Mungu na Mwanaye, Yesu Kristo, halafu ayatendeshe kazi katika mazoea. (Yohana 17:3) Kusikia hivyo, yeye akakubali funzo la nyumbani la Biblia. Leo, yeye anatumikia Yehova akiwa mmoja wa mashahidi wake.

Wengi wa wale ambao wamekubali ukweli ni wa kutoka nchi nyinginezo. Wao wamefanya Cayman ikawa maskani yao au wao ni wakaaji wa muda wenye kazi za mikataba. Hivyo, dada mmoja alitaja kwamba ana tamaa ya kuona wenyeji wengi zaidi wa Cayman wakiwa katika kundi. Yeye alisali kwa Yehova ili amsaidie kupata mwenyeji mwenye kutaka kujifunza Biblia. Muda usio mrefu baada ya hapo, yeye alifikia mwanamke kijana aliyekuwa tayari ana kitabu Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele, na dada yule akaanza funzo la Biblia pamoja naye. Katika muda wa miezi michache, mwanamke huyo alianza kuhudhuria mikutano, akaacha dini yake ya zamani, na kuanza kushiriki pamoja na wengine mambo aliyokuwa anajifunza. Katika muda wa mwaka mmoja akawa shahidi wa Yehova aliyejiweka wakfu na kubatizwa.

Kazi ya kuhubiri ilipokea kichochezi zaidi katika 1982, wakati mume na mke wamisionari walipogawiwa kwenda Grand Cayman. Wao waliongoza mafunzo mengi ya nyumbani ya Biblia na kuweka msingi mzuri wa mpanuko zaidi.

Upinzani Washindwa Katika Cayman Brac

Kisiwa cha Cayman Brac kiko karibu kilometa 140 kaskazini-mashariki mwa Grand Cayman. Mara kwa mara, wamisionari na wafanya kazi wengine wa wakati wote kutoka Grand Cayman walitua kidogo penye kisiwa hicho ili kuwaletea habari njema wakaaji wacho 1,700. Lakini mambo ya kutaharukisha yakaanza kutukia katika 1986.

Mume na mke mmoja wenye kufanya kazi ya mkataba huko walianza kujifunza na kufanya maendeleo kufikia hatua ya kujiweka wakfu na kubatizwa. Ndipo, Mashahidi wengine wawili wakahamia huko kutoka mabara mengineyo. Baada ya muda mfupi ule utendaji ulioongezeka ukaleta hasira kuu ya wapinzani, ambao walijaribu kufanya wakuu wenye kuhusika na uhamiaji-nchi wafute ruhusa za kikazi za mume na mke waliobatizwa karibuni. Hata hivyo, jitihada zao zilisukumwa kando wakati mkuu wa maafisa wa uhamiaji-nchi katika Georgetown, Grand Cayman, alipochukua msimamo wa kwamba ikiwa wapinzani wa kidini waliudhiwa na kazi ya Mashahidi, inawapasa wao pia waende nyumba kwa nyumba ili waipinganishe. Tangu hapo hakuna uhasama wowote wa waziwazi ambao umehisiwa.

Wakumbukwa na Yehova

Kwa uhakika watu wa Visiwa vya Cayman wamekuwa hawakusahauliwa na Yehova, yule Muumba Mwadhamu. Bali, yeye anafanya iwezekane habari njema kuhubiriwa katika visiwa hivyo vidogo, hiyo ikiutimiza unabii wa Isaya: “Mwimbieni BWANA [Yehova, NW] wimbo mpya, na sifa zake tokea mwisho wa dunia; ninyi mshukao baharini, na vyote vilivyomo, na visiwa, nao wakaao humo.”​—Isaya 42:10.

Visiwa vya Cayman vinaweza kushangilia kwamba kutokana na kituo cha msimamo wa Yehova, hivyo si “Visiwa Vilivyosahaulika Baada ya Muda Kupita.”

[Ramani katika ukurasa wa 22]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Bahari Karibea

LITTLE CAYMAN

CAYMAN BRAC

[Map]

GRAND CAYMAN

[Map]

CUBA

LITTLE CAYMAN

GRAND CAYMAN

CAYMAN BRAC

JAMAICA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki