‘Mimi Sikutarajia Kukionea Shangwe’
HIVYO ndivyo mtu mmoja alivyoandikia rafiki aliyekuwa amempelekea nakala-zawadi ya kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? “Mimi nina uhakika umetaka kujua kama nilipata kitabu hicho,” mtu yule akaandika. “Ndiyo! Asante! Je! nilikisoma? Jibu ni ndiyo pia. Nilishangaa sana kukipata kikiwa cha kusisimua.
“Sikutarajia hata kidogo kukionea shangwe, kwa kweli, nilianza kukisoma ili niweze kukuambia wewe ‘Ni sawa tu, nilikijaribu.’ Mambo hayakwenda nilivyotarajia kwa maana sikuweza kukiweka kando. . . . Labda ilinichukua siku 10 kukimaliza. Niliduwaa kwa furaha. Upesi nikasimulia baadhi ya rafiki zangu habari za kitabu hicho—nikaazima wawili wawe nacho na kuahidi kumwazima wa tatu! Kwa hiyo angalau sisi 4 tutakisoma, na ninatarajia wengine zaidi watakisoma pia. Ni kitabu kizuri kweli kweli. Kwa mara nyingine tena, asante.”
Je! wewe unajua mtu fulani ambaye ungeweza kupelekea kitabu ambacho angekionea shangwe kikweli? Basi kwa nini usimpelekee nakala-zawadi ya Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Unaweza kufanya hivyo kwa kujaza tu na kutupelekea hati yenye anwani iliyopo chini, na kupeleka Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00) pamoja nayo.
Tafadhali pelekeni, mkiwa mmelipia malipo ya posta, nakala-zawadi ya kile kitabu cha kurasa 256 Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? na pia barua yenye kueleza kwamba ni zawadi kutoka kwa (jina lako). Mimi nawapelekea nyinyi Kshs. 40.00 (Tshs. 200.00).