Si kwa Ajili ya Watoto Tu
Mwanamke mmoja wa kutoka Fort Worth, Texas, anaandika hivi: “Mimi nimekuwa na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu kwa miaka kadhaa. Niliamua kuanza kumsomea mwana wangu wa miezi kumi kitabu hicho. Kila siku nasoma sura mbili au tatu.
Najua kwamba yeye angali mchanga mno kukielewa. Hata hivyo, kimeninufaisha sana mimi binafsi. Kitabu hicho kiligusa moyo wangu kwa njia ya pekee sana na kikaongezea kina cha upendo na uthamini wangu kwa Yehova Mungu na Mwana wake, Yesu Kristo. Mimi nina miaka 27. Nilifikiri kitabu Mwalimu Mkuu ni kwa ajili ya watoto tu, na sasa nasikitika kwamba sikutazama ndani mapema zaidi.”
Wewe utapelekewa kitabu hiki chenye jalada gumu cha kurasa 192 kwa Kshs. 15/= (Tshs. 80/=; RWF 100) tu. Njia nyingine ni kwamba, kwa Kshs. 180/= (Tshs. 1,200/=; RWF 2,000) unaweza sasa kupata kitabu hicho na mrekodi wacho katika kanda za kaseti nne zikiwa katika pakiti ya kupendeza.
Tia alama katika sanduku linalofaa na upeleke mchango ulio sahihi:
[ ] Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, kile kitabu
chenye jalada gumu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu; mimi nawapelekea Kshs. 15/= (Tshs. 80/=.
[ ] Tafadhali mnipelekee, mkiwa mmelipia malipo ya posta, ile pakiti laini yenye rangi ya kupendeza pamoja na kaseti nne na kitabu Kumsikiliza Mwalimu Mkuu (kwa Kiingereza). Mimi nawapelekea Kshs. 180/=.