Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 10/1 uku. 31
  • Ukimwi Je! Ni ‘Mwanzo wa Adili Mpya’?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukimwi Je! Ni ‘Mwanzo wa Adili Mpya’?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 10/1 uku. 31

Ukimwi Je! Ni ‘Mwanzo wa Adili Mpya’?

BAADA ya kuonyesha wazi kwamba daktari wa kitiba alikuwa amesema kwamba “uhusiano pamoja na mwenzi mmoja tu wa ndoa” ndiyo njia pekee ya kuepuka kupata UKIMWI wenye kuambukizwa kingono, Mkanada aliye mwandikaji wa tahariri aliuliza hivi: “Je! ule UKIMWI wenye kuhofiwa sana ungeweza kuwa ndio mwanzo wa adili mpya kabisa katika ulimwengu wetu?” Mwandikaji huyo alishangaa, pia, kama si “ajabu” kwamba jambo lile ambalo Biblia imefundisha kwa miaka kadhaa, yaani, kuwa na mwenzi mmoja tu wa ndoa, “lingeweza sasa kuokoa uhai wa aina ya binadamu.” Ikiurejezea pia ulimwengu wa leo wa “dawa za kulevya, tumbako, kileo na nyege za kupita kiasi, ambazo si jambo dogo,” tahariri hiyo ilisema: “Sasa sisi tunalipa bei ya ulimwengu wa picha za umalaya, wa ngono za ovyoovyo na wenye uchafuzi ambao sisi tumeufanyiza.”

Ingawa ni vema kutumainia kuwe na maendeleo katika mwenendo na kuendelea kuwa hai, je! hofu ya kifo cha mapema au ya mwisho wa aina ya binadamu ndiyo itatokeza “adili mpya kabisa”? Sivyo, kwa maana kujapokuwa na maonyo kutoka kwa madaktari na watafiti, walio wengi wa wavutaji sigareti na wanywaji wa kileo huendelea kipumbavu kupuuza afya yao, wakileta maisha zao kwenye mwisho wa mapema mno. Na baadhi ya wagoni-jinsia-moja wametaarifu kwamba wataendelea kuwa na wenzi wengi hata kwa kujasiria kupata UKIMWI,—Mithali 10:21, 23.

Basi, ni kitu gani kitazuia makosa kwa njia ifaayo? Kwa uhakika, ni hofu yenye afya na staha kwa Yehova, ambayo huonwa kwa kutii sheria zake kuhusu adili. “Hofu kwa Yehova ndio mwanzo wa maarifa.” Na maarifa ya aina hii hutokeza hekima ambayo kwa kweli “huhifadhi hai walio nayo.”—Mithali 1:7; Mhubiri 7:12, NW.

Jambo la umaana mkubwa ni kwamba, mhariri yule akiwa anatoa arifa ya kwamba UKIMWI waweza kupatwa kupitia kutiwa damu mishipani, aliuliza hivi pia: “Je! si jambo la kinyumenyume kwamba sisi ambao tumewashutumu kabisa Mashahidi wa Yehova kwa kukataa kutiwa damu mishipani . . . huenda sasa tukawa tunafanya jambo lile lile kwa sababu nyinginezo?”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki