Mimi Ningefurahi Kuichagua Amkeni!
Ndivyo alivyoandika Frank Senge katika Post-Courier ya Papua New Guinea. Katika safu yake ya kila juma ya Julai 19, 1988, Senge alieleza hivi:
“Ukurasa wa yaliyomo [katika Amkeni!] hueleza kwamba gazeti hilo hutangazwa kwa chapa ili kuipa jamaa nzima nuru ya elimu.’
“‘Huonyesha jinsi ya kukabiliana na matatizo ya leo,’ hilo lasema.
“Nalo hufanya hivyo hasa. Tofauti na barua-habari au magazeti mengine mengi ya makanisa, Amkeni! hueleza kuhusu Mungu kupitia matatizo ya kilimwengu yanayotuzunguka.
“Huenda hii ikaonekana kama propaganda ya kidini (mimi si [Shahidi]) . . . lakini kama tungepaswa kuamua ufaaji wa magazeti, kwa ajili ya jamaa, mimi ningefurahi kuichagua Amkeni!”
Sisi twahisi kwamba wewe pia utaona shangwe ya kuwa na Amkeni! Gazeti hilo lina chapwa kwa wastani wa nakala 11,250,000 kila nakala na hutangazwa kwa chapa katika lugha 54.
Tafadhali mnipelekee andikisho la mwaka mmoja la Amkeni! Mimi nawapelekea Kshs. 45/= (Tshs. 300/=) kwa matoleo 12 ya gazeti hili (nakala 1 kwa mwezi).