Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 11/1 uku. 15
  • ‘Nena Neno la Mungu kwa Ujasiri’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Nena Neno la Mungu kwa Ujasiri’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Mwige Yesu—Hubiri Kwa Ujasiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • ‘Sema Neno la Mungu kwa Ujasiri’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Endelea Kusema Neno la Mungu kwa Ujasiri
    Huduma ya Ufalme—2005
  • Ujasiri
    Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 11/1 uku. 15

‘Nena Neno la Mungu kwa Ujasiri’

YEHOVA Mungu aweza kuwatia nguvu watumishi wake ‘wanene Neno la Mungu kwa ujasiri.’ (Matendo 4:31, NW) Hata wale walio wachanga katika njia za ukweli wa Biblia na wasio na ujuzi katika utendaji wa kueneza evanjeli hawahitaji kusita kunena habari njema kwa ujasiri. Katika Cote d’Ivoire, wahubiri wawili wa habari njema walikuwa katika huduma ya mlango kwa mlango walipokutana na profesa wa chuo kikuu. Shahidi aliye mchanga zaidi, Seriki, kwa kuhisi hakuwa na sifa za kumstahilisha kunena na mwanamume mwenye elimu jinsi hiyo, aliacha Shahidi yule mwingine aongee.

Profesa huyo alifadhaishwa na ubaguzi wa rangi naye akalaumu Mungu kwa matatizo yaliyopo ya kubagua rangi, akihisi kwamba yeye ndiye aliyeumba zile rangi tofauti za watu. Baada ya zungumzo refu lililoonekana kutotimiza lengo lolote, mwishowe Seriki alipiga moyo konde kwamba atanena, na kwa uungwana akakatiza maongeo hayo. (1 Wathesalonike 2:2) Kwa kuona kwamba nyumba ya profesa huyo ilipambwa kwa rangi za kupendeza sana, Seriki akamuuliza profesa, “Kwa nini wewe hukufanya nyumba yako yote iwe ya rangi moja?”

“Wewe wafikiri mimi mjinga sana, eh!” profesa huyo akajibu kwa ukali. Naye Seriki akajibu: “Hapana, lakini mbona sisi tutarajie Mungu afanyize kila kitu na kila mtu akiwa wa rangi ile ile moja?” Wazo lile likaeleweka wazi. Kielezi hicho sahili kilithibitika kuwa chenye matokeo, na ushahidi mzuri ukatolewa na Seriki huyo ambaye hapo kwanza alikuwa mwoga-mwoga.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki