Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lmd somo la 6
  • Ujasiri

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ujasiri
  • Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Alifanya Nini?
  • Tunajifunza Nini Kutoka kwa Yesu?
  • Mwige Yesu
  • Mwige Yesu—Hubiri Kwa Ujasiri
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Je, Wahubiri kwa Ujasiri?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2000
  • ‘Sema Neno la Mungu kwa Ujasiri’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Endelea Kusema Neno la Mungu kwa Ujasiri
    Huduma ya Ufalme—2005
Pata Habari Zaidi
Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
lmd somo la 6

KUANZISHA MAZUNGUMZO

Yesu anamsihi Zakayo ashuke chini, huku baadhi ya watu wakishangaa.

Luka 19:​1-7

SOMO LA 6

Ujasiri

Kanuni: “Tulijipa ujasiri kupitia Mungu wetu ili tuwatangazie ninyi habari njema ya Mungu.”—1 The. 2:2.

Yesu Alifanya Nini?

Yesu anamsihi Zakayo ashuke chini, huku baadhi ya watu wakishangaa

VIDEO: Yesu Anamhubiria Zakayo

1. Tazama VIDEO, au soma Luka 19:​1-7. Kisha fikiria maswali yafuatayo:

  1. Kwa nini baadhi ya watu waliepuka kushirikiana na Zakayo?

  2. Ni nini kilichomchochea Yesu amhubirie habari njema?

Tunajifunza Nini Kutoka kwa Yesu?

2. Tunahitaji ujasiri ili tuhubiri ujumbe wa Ufalme bila ubaguzi.

Mwige Yesu

3. Mtegemee Yehova. Roho ya Mungu ilimpa Yesu nguvu za kuhubiri, na inaweza kukusaidia pia. (Mt. 10:​19, 20; Luka 4:18) Mwombe Yehova akupe ujasiri wa kuwahubiria watu unaowaogopa.—Mdo. 4:29.

4. Usiwahukumu watu. Huenda tukasita kuzungumza na baadhi ya watu kwa sababu ya mwonekano wao, cheo chao katika jamii au hali yao ya kiuchumi, mtindo wao wa maisha, au dini yao. Lakini kumbuka:

  1. Yehova na Yesu wanaweza kusoma mioyo; sisi hatuwezi.

  2. Tusihisi kwamba mtu huyo hawezi kusaidiwa na Yehova.

5. Uwe jasiri lakini mwenye busara na tahadhari. (Mt. 10:16) Epuka kubishana. Maliza mazungumzo kwa upole ikiwa mtu hataki kusikiliza habari njema au unahisi hauko salama.—Met. 17:14.

SOMA PIA

Mdo. 4:31; Efe. 6:​19, 20; 2 Tim. 1:7

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki