“Kichapo Kifanywacho na Mashahidi wa Yehova Chastahiki Kusomwa”
Hiki kilikuwa kichwa cha makala iliyotokea siku ya Desemba 23, 1988, katika Creston News Advertiser, ya Iowa, U.S.A. “Falsafa na dini hunipendeza mimi,” asema mwandikaji-mwanakazi Randy Porter, “lakini vichapo hivyo vina hadithi fulani ambazo nusu yazo ni za mambo ya ulimwengu yahusuyo unamna-namna wa kustaajabisha juu ya masuala ya ulimwengu. . . .
“Zaidi ya hilo, huenda watu fulani wakashangaa kujua kwamba mara nyingi magazeti hayo hunukuu vyanzo vingine vya kimamlaka, mbali na Biblia. . . .
“Kwa habari hiyo, Chapa ya Januari [22] yakazia pia hadithi fupi na fotografu yenye rangi ya mwamba wa kitaifa wa Iowa, lile jiwe angavu la jiodi. Makala hiyo yasema kwamba watu ni kama mawe maangavu ya jiodi. Ingawa kwa nje yaonekana kuwa na sura ya kikawaida tu, mawe maangavu ya jiodi yafunguliwapo hufunua uzuri wa kindani wenye uangavu mwingi wa kustaajabisha. Huenda pia mtu akaonekana kuwa mwenye sura ya kikawaida nje-nje, na hata mnyamavu na mwenye haya-haya; hata hivyo, mtu achukuapo ‘wakati wa kuzoeana naye, mtu huyo hufungulia maoni yake na kukuonyesha uzuri wa kindani wenye kutokeza mwanga.’ . . .
“Toleo la Januari [22] lilikuwa na makala nyingine nyingi pia ambazo labda zisingaliweza kufikia dawati langu! Kwa kielelezo, watu walio wengi wamesikia habari za nyuki wauaji wa Kiafrika, lakini makala moja ilisimulia jinsi wanamazingira wanavyotega kinasa-sauti katika nyuki hao. Hicho chombo kidogo sana cha kupeleka habari ambacho udogo wacho watosha kushikanishwa na tako la nyuki kitawezesha wanasayansi kufuatisha miendo ya nyuki kuanzia kilometa moja hadi mbili.”
Amkeni! ina waleta-habari katika nchi nyingi kuzunguka ulimwengu na kwa hiyo ina vyanzo vya habari ambavyo wengi hawawezi kuwa navyo. Sisi twahisi kwamba wewe waweza kunufaika kuona shangwe kutokana na makala zinazosisimua za Amkeni! Wastani wa kuchapwa kwa gazeti hilo ni nakala 11,250,000 kwa toleo na latangazwa kwa chapa katika lugha 53.
Tafadhali nipelekeeni andikisho la mwaka la Amkeni! Mimi nawapelekea Kshs. 45/= (Tshs. 300/=) kwa matoleo 12 ya gazeti hili (nakala 1 kwa mwezi).