Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 11/15 kur. 30-31
  • Ghasia za Umati Haziwezi Kuzuia Habari Njema

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ghasia za Umati Haziwezi Kuzuia Habari Njema
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 11/15 kur. 30-31

Ghasia za Umati Haziwezi Kuzuia Habari Njema

SIKU moja ya Februari uliopita, habari mpya zilizotazamiwa kwa muda mrefu kuhusu uchumi wa Venezuela zilitangazwa. Bei zilikuwa zikiinuliwa kwa asilimia zaidi ya 100 kuhusu vyakula vile vya msingi kama maziwa, unga, na mkate. Bei za petroli zingeongezeka kwa asilimia 90. Nauli za usafiri ziliidhinishwa kupanda kwa asilimia 30. Nchi hiyo ikashangaa sana. Kwa gafula, siku ya Jumatatu, Februari 27, watu walijibu kitendo hicho kwa kufanya ghasia za umanti katika taifa lote.

Asubuhi iliyofuata, mambo yakawa yamefikia hatua kubwa ya uharibifu na uporaji. Milio ya bunduki ilisikiwa-sikiwa katika mahali kadhaa. Vijana kwa wazee walipita kwa fujo nyingi katika barabara za jiji, wakiacha nyuma yao dalili za uharibifu uliofanana na uwanja wa pigano ulioharibiwa sura na vita.

Alasiri hiyo rais wa nchi alijulisha rasmi kwamba nchi imepatwa na hali ya dharura na akaachisha haki za kikatiba kwa siku kumi. Likaanzishwa amrisho la kwamba watu wawe nyumbani kati ya saa 12 jioni na 12 asubuhi. Siku iliyofuata, waziri wa ulinzi alitangaza kwamba amrisho hilo lingeendelea kutumika mpaka arifa zaidi itolewe. Wanajeshi walitumia mamlaka yao kudhibiti mabarabara, kuingia nyumba za watu bila kuidhinishwa, na kusimamisha watu na kuwapekua. “Watu mia mbili wafa na elfu moja wajeruhiwa muda wa siku tatu za machafuko,” ikaripoti karatasi-habari moja.

Makundi ya Mashahidi wa Yehova yalikuwa na hali gani wakati wa mzozo huu? Akina ndugu walishauriwa hivi: Mwe wenye busara na mwepuke maeneo yenye matata. Rekebisheni nyakati za mikutano ili zipatane na amrisho la saa za kuwa nyumbani, na mwepuke kuhubiri mkiwa vikundi vikubwa-vikubwa. Hata hivyo, kuhubiriwa kwa habari njema za Ufalme wa Mungu kulisonga mbele.—Mathayo 24:14; 28:19, 20.

Kwa sababu mume asiyeamini wa mwana-mke mmoja Mkristo alikuwa na wasiwasi kuhusu hali njema yake kama mwanamke huyo angekanyaga nje ya nyumba akahubiri, alimkataza asiondoke. “Wewe huelewi kwamba mimi nina wajibu wa kutimiza,” mwanamke huyo akamwambia. “Haya basi! Mimi nitajifunza Biblia pamoja nawe!”

Hii ndiyo mara ya kwanza katika miaka ile 22 ya mwanamke huyo kuwa Shahidi kwamba mume wake alionyesha nia ya kujifunza Biblia. Lakini mume huyo alitahadharisha hivi: “Ni sawasawa, maadamu wewe waahidi kutoenda nje. Lakini usiniuliza maswali, nisomee tu.” Hata hivyo, dada yule alijifunza naye muda wa saa moja na nusu. “Lilikuwa funzo la kiolezo bora kabisa, funzo bora kuliko yote ambayo nimepata kuwa nayo miaka yangu 22 ya kuwa katika ukweli,” akasema mwanamke huyo, huku akilengwa-lengwa na machozi machoni.

Katika kisa kingine, painia wa kawaida alikuwa akifagia kijia cha nje ya nyumba yake alipofikiwa na bibi mmoja aliyekuwa hataki kuwasikiliza Mashahidi walipozuru nyumba yake. “Mimi sijawaona nyinyi Mashahidi mkihubiri hivi karibuni,” akasema mwanamke huyo. “Usiniambie kwamba nyinyi hamtahubiri tena!”

Dada akaeleza kwamba walikuwa wameacha kuhubiri nyumba kwa nyumba wakati ule tu wa ghasia za umati. “Lakini siku itafika ambapo sisi hatutahubiria watu tena, na hiyo itamaanisha mwisho wa ulimwengu,” akasema dada huyo. “Yakupasa wewe ujifaidi na fursa iliyopo sasa na kukubali funzo la Biblia katika nyumba yako.”

“Twaweza kufanya mipango lini?” bibi huyo akauliza kwa haraka. Papo hapo mipango ikafanywa kuanzisha funzo la nyumbani la Biblia.

Shukrani ni kwamba msukosuko ule ulikoma, hiyo ikaruhusu mambo ya nchi yarudie kawaida. Hata hivyo, katika hali hizo za wasiwasi mwingi, ni faraja kujua kwamba karibuni utakuwapo ulimwengu mpya wenye utulivu mwingi na usalama. Neno la Mungu laahidi hivi: “Ziko mbingu mpya na dunia mpya ambazo sisi tunangojea kulingana na ahadi yake, na katika hizo uadilifu utakaa.” (2 Petro 3:13, NW) Na maadamu Mungu aruhusu, Mashahidi wa Yehova wataendelea kuzihubiri habari njema za Ufalme.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Msukosuko haukusimamisha wapiga mbiu ya Ufalme

[Hisani]

Fotografu imetolewa na Publicaciones Capriles, Caracas, Venezuela.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki