Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 1/15 uku. 32
  • Yeye Alivutiwa Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yeye Alivutiwa Sana
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 1/15 uku. 32

Yeye Alivutiwa Sana

Alipokuwa akisafiri katika gari-moshi la chini ya ardhi katika New York masika yaliyopita, mwanamke mmoja kijana alikuwa akisoma kitabu Revelation​—Its Grand Climax At Hand! Mwanamume aliyeketi karibu naye aliona kichapo hicho, na mwanamke yule alipokuwa akifungua-fungua kurasa zacho, mwanamume huyo alivutwa sana na zile picha za kupendeza sana. “Lo, hakika kitabu hicho chaonekana kuwa cha kupendeza sana!” yeye akasema.

“Naam, ndivyo kilivyo,” mwanamke huyo akaitikia. “Chaeleza kitabu cha Biblia cha Ufunuo, sura kwa sura.”

“Naweza kupataje kimoja cha hivyo?” mwanamume huyo akataka kujua.

“Kutoka kwa Mashahidi wa Yehova,” mwanamke yule akaitikia. Lakini ndipo akaendelea kusema: “Wajua, nakala hii niliyo nayo ni mpya, nayo ni ya dola 3 tu, kwa hiyo ningeweza kukuacha uwe nayo.”

‘Mara ile ile mwanamume huyo akatoa pesa hizo mfukoni mwake na kukubali kitabu kile. Pale pale, gari-moshi likasimama, naye akapaswa kuharakisha.

Kitabu hiki cha kuvutia sana kilicho na jalada gumu, chenye kurasa za ukubwa ulio sawa na gazeti hili, chatoa ufikirio wa mstari kwa mstari wa kitabu kizima cha Biblia cha Ufunuo. Chaandaa utambulisho ulio wazi, wa kutumia hoja nzuri za kueleza juu ya wale hayawani, yule drakoni, yule kahaba mkubwa, na zile sehemu nyingine za ufananisho za Ufunuo. Utaiona maana kwa siku yetu. Peleka habari leo ili ukipokee.

Tafadhali mnipelekee kile kitabu cha kurasa 320 Revelation​—Its Grand Climax At Hand! Mimi nawapelekea Kshs. 60/= (Tshs. 360/=; RWF 300).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki