Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 2/1 uku. 3
  • Wewe Waweza Kuiamini Biblia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wewe Waweza Kuiamini Biblia?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Mageuzi Yajaribiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Je, Niamini Mageuzi?
    Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Uumbaji au Mageuzi?—Sehemu ya 1: Kwa Nini Nimwamini Mungu?
    Vijana Huuliza
  • Mageuzi
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 2/1 uku. 3

Wewe Waweza Kuiamini Biblia?

“NI SALAMA kabisa kusema kwamba ukikuta mtu fulani ambaye adai kutoamini mageuzi, mtu huyo ni mkosa-maarifa, ni mjinga au hana akili timamu.” Wewe waathiriwa jinsi gani na maneno haya yaliyosemwa na mwanabayolojia Richard Dawkins? Ikiwa wewe waiamini Biblia, yaelekea waamini uumbaji badala ya ile nadharia ya mageuzi. Je! hiyo yamaanisha kwamba, ukiwa mwamini katika Biblia, wewe ni mkosa-maarifa, mjinga, au huna akili timamu?

Fikiria, pia, taarifa hii: “Wanachuo wa Agano Jipya wamethibitisha kwa njia isiyoweza kutiliwa shaka lolote la kiakili kwamba Yesu yule atajwaye na hati za Kikristo si mtu wa kihadithi tu ambaye huwa akiwaziwa na Wakristo.” Maneno haya yaliyo katika The Weekend Australian yalinenwa na Dakt. Robert W. Funk, profesa wa chuo kikuu wa uchunguzi wa kidini, aliye mtungaji wa hesabu fulani ya vitabu ambavyo vyahusu fasiri ya kidini.

Dakt. Funk alianzisha mradi ujulikanao kuwa Warsha ya Yesu, kikundi cha wanachuo wa Biblia zaidi ya mia moja ambao wakiwa pamoja walizichunguza sana semi za Yesu zilizoripotiwa katika Biblia. Miongoni mwa mambo mengi, walikata shauri kwamba Sala ya Bwana haikutungwa na Yesu; kwamba Yesu hakusema kwamba wasikivu wangerithi dunia wala kwamba wafanyiza-amani (wapatanishi, UV) wangeitwa wana wa Mungu; na kwamba hakusema: “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi . . . hatakufa kabisa.”​—Yohana 11:25, 26; Mathayo 5:5, 9; 6:9, 10.

Hata ingawa huenda ukagutushwa na vile walivyokata maneno, hayo si mambo yasiyo ya kawaida. Yametokana na uchambuzi wa ki-siku-hizi ufanywao kuhusu Biblia, na mawazo kama hayo yamefundishwa katika seminari za kidini kwa muda fulani. Labda wewe umejishupaza usiathirike kwa kusikia Biblia ikipinganishwa na wanasayansi. Lakini wakati viongozi wa kidini watiapo shaka juu ya ukweli wa kumbukumbu la Biblia, huenda ukajiuliza kama wewe sasa wapaswa kufikiria upya msimamo wako mwenyewe. Je! ni jambo la kiakili kuamini Biblia hali yaonekana wazi kwamba watu wengi sana wenye akili katika uwanja wa kidini hawafanyi hivyo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki