Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 2/15 uku. 24
  • Kodeksi Bezae Hatimkono Isiyo na Kifani

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kodeksi Bezae Hatimkono Isiyo na Kifani
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kodeksi ya Vatikani—Kwa Nini Ni Yenye Thamani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Fumbo la Kodeksi ya Vatikani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kodeksi ya Alexandrine
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Tarehe ya Hati za Zamani Hujulikanaje?
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 2/15 uku. 24

Kodeksi Bezae Hatimkono Isiyo na Kifani

Theodore de BEZE, mwanachuo Mfaransa mashuhuri kuhusu Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, alikuwa mshirikiani wa karibu na mwandamizi wa mrekebisha-kanisa Mprotestanti John Calvin. Katika mwaka 1562, Beza, kama vile yeye huitwa na wengi zaidi, alivumbua hatimkono moja ya kale isiyo ya kikawaida. Alidai kuwa aliipata kutoka kwenye makao ya utawa ya “Mtakatifu” Irenayo katika Lyons, Ufaransa, baada ya jiji hilo kuporwa vibaya sana na Wahugwenoti [Wafaransa Waprotestanti]. Mahali pa asili yayo si dhahiri, lakini yaelekea zaidi kwamba Afrika Kaskazini au Misri ndilo chimbuko layo.

Kodeksi hiyo ina vipimo vya sentimeta 25 kwa 20 na kwa ujumla hukiriwa kuwa ya tarehe ya kuanzia karne ya tano W.K., baadaye kidogo kuliko zile hatimkono za Sinai, Vatikani, na Aleksandrini. Ina sahifa (kurasa) 406 na ina Gospeli zile nne tu na Matendo ya Mitume, kukiwa na mapengo fulani. Lakini Kodeksi Bezae huenda ikawa hapo awali ilitia ndani barua nyinginezo, kwa maana kuna kigereng’enza cha barua ya tatu ya Yohana. Gospeli za Mathayo na Yohana hutangulia zile za Luka na Marko.

Hatimkono hiyo ni kielelezo cha mapema cha matini (maandishi-awali) ya lugha mbili, huku Kigiriki kikiwa katika ukurasa wa kushoto na Kilatini katika wa kulia. Labda hiyo ni nakala ya hatimkono ya funjo yenye matini ya mapema, yenye kufanana na mafunjo mengine ya karne za tatu au nne ambazo zajulikana kuwa P29, P38, na P48.

Ikiwa imeandikwa kwa herufi kubwa za kupendeza, Kodeksi Bezae haikuandikwa kwa mistari yenye uendelevu katika kurasa. Imepangwa katika mistari isiyolingana urefu, hivi kwamba mwisho wa kila mstari huwakilisha kituo katika usomaji. Ni ajabu kwamba Kilatini hicho kimeandikwa kwa mtindo wa mpangilio wa herufi za Kigiriki, na matini imerekebishwa ilingane na misomo ya Kigiriki katika visa vingi. Kwa upande ule mwingine, matini ya Kigiriki ni pambanufu sana na imesahihishwa na mikono mingi, kutia na ile ya mwandishi wa awali.

Kodeksi Bezae ina mtajo rasmi wa “D.” Yatofautiana sana na hatimkono nyinginezo zote zilizo kubwa-kubwa na kujitegemea bila hizo. Kama ionyeshwavyo na vielezo-chini katika New World Translation of the Holy Scriptures, kodeksi huwa haiafikiani nyakati fulani na zile Kodeksi Sinai (א), Vatikani (B), na Aleksandrini (A). Thamani kubwa ya kodeksi hii imo katika uthibitisho ambao yatoa kuhusu hatimkono nyingine za maana wala si katika zile namna zayo za pekee za kuondoa na kuongezea mambo fulani.—Ona vielezo-chini katika New World Translation of the Holy Scriptures —With References, kwenye Mathayo 23:14; 24:36; 27:49; Marko 7:16; 9:44, 46; 11:26; Luka 15:21; Yohana 5:4.

Kujapokuwa na misomo na mitofautiano fulani isiyo ya kawaida, Kodeksi Bezae ni ushuhuda mwingine wa kuhifadhiwa kwa Biblia mpaka siku yetu.

[Hisani wa picha katika ukurasa wa 24]

Juu: Kwa ruhusa ya Mawakili wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Cambridge

Kushoto: Kwa hisani ya Wadhamini wa British Museum

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki