Amkeni! Lathaminiwa kwa Mapana
Amkeni! hutangazwa katika lugha 55, na huchapwa kwa wastani wa nakala 11,930,00 kila toleo. Wasomaji kuzunguka ulimwengu hulionea shangwe na kunufaika nalo, kama ifunuliwavyo na barua zao za uthamini. Ofisi ya tawi la Mnara wa Mlinzi katika Thailandi ilipokea ombi linalofuata:
“Shule yetu inapokea kwa ukawaida gazeti Amkeni! [la Kithai], nasi twaona kwamba toleo la Septemba 8, 1988, laihusu habari ‘Wazazi,’ ambayo wazazi wote wenye watoto wa shule wapaswa kusoma. Kwa hiyo tungependa nyinyi mtupelekee nakala 250,400 ikiwa zipo ili zigawanywe kwenye mkutano ufuatao wa wazazi na walimu.”
Mwanamke mmoja kutoka Roanoke, Virginia, U.S.A., aandika hivi: “Mimi ni Mbaptisti mwenye ujitoaji mwingi nikiwa mshiriki humo, lakini nilipata moja ya karatasi-habari zenu Amkeni! katika madobini jirani na nimenurishwa sana. Nimeona shangwe kuisoma. Ndani ya bahasha hii ninatia [hundi ya dola 5], na kwa hiyo mnipelekee andikisho la mwaka mmoja la Amkeni!”
Sisi twahisi kwamba wewe pia utanufaika na kuzionea shangwe makala za kusisimua zilizo katika Amkeni!