Kitu Bora Kuliko Televisheni
Mama mmoja kutoka Indianapolis, Indiana, U.S.A., aandika kwamba ametoka sasa tu kuagizia mwanaye wa miaka minne seti ya pili ya kanda za kaseti za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mama huyo aungama hivi: “Mara nyingi sisi, baba yake na mimi, tuwapo tukitazama televisheni katika sebule, yeye huwa jikoni akiwa amefungulia na kusikiliza hadithi za Biblia. Hiyo hutusumbua sana mpaka tunafunga televisheni.”
Mama huyo amalizia hivi: “Twahisi uhakika wa kwamba kanda za Hadithi za Biblia zimemsaidia kuwa kivulana mtulivu zaidi na mwenye furaha zaidi. . . . Asanteni sana.”
Kusikiliza kaseti za hadithi 116 zilizo katika Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia ni njia nzuri sana kwa wachanga kujifunza Biblia yahusika na nini hasa. Ikiwa mtoto mchanga ana upendezi aweza kukumbuka mengi kuliko ufikirivyo. Jamaa nyingi zimepata Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, pamoja na mrekodi wa kitabu hicho katika kanda za kaseti, kuwa ndicho kitu kile hasa chenye kuhitajiwa ili kuchochea upendezi huo. Wewe waweza kupokea hizo kanda za kaseti au lile buku Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, au vyote viwili, kwa kujaza na kutupelekea hati ya anwani iliyopo chini.
Tia alama katika sehemu moja au zote mbili zifuatazo, na ulipe mchango ulio sahihi:
□Tafadhali nipelekeeni ile albamu vainili ya kahawia yenye kanda za kaseti nne za Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia. Mimi nawapelekea Kshs. 190/= (Tshs. 960/=.).
□Tafadhali nipelekeeni Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia cha kurasa 256, ambacho kwacho mimi nawapelekea Kshs. 190/= (Tshs. 960/=.).