Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 4/15 kur. 8-9
  • Wale Wanawali Wenye Hekima na Wapumbavu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wale Wanawali Wenye Hekima na Wapumbavu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Nuru ya Elimu Wakati wa “Umalizio wa Mfumo wa Mambo”
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
  • Somo Kuhusu Kuwa Macho​—Mabikira
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Hakuna “Upungufu wa Nguvu” wa Kiroho kwa Wenye Busara
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Kulinda Wakati wa “Umalizio wa Mfumo wa Mambo”
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 4/15 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Wale Wanawali Wenye Hekima na Wapumbavu

YESU amekuwa akijibu ombi la mitume wake la ishara ya kuwapo kwake katika mamlaka ya Ufalme. Sasa anaandaa mambo zaidi ya ishara kwa mifano au vielezi vitatu.

Utimizo wa kila kielezi kimojapo ungeonwa na wale wanaoishi wakati wa kuwapo kwake. Yeye atanguliza cha kwanza kwa maneno haya: “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara.”

Kwa usemi ‘ufalme wa mbinguni utafanana na wanawali kumi,’ Yesu hamaanishi kwamba nusu ya wale watakaorithi ufalme wa mbinguni ni wapumbavu na nusu ni wenye busara! Hapana, lakini anamaanisha kwamba kuhusiana na Ufalme wa mbinguni, kuna upande ulio hivi au ulio vile. Au kwamba mambo kuhusiana na Ufalme yatakuwa kama kitu fulani fulani.

Wanawali kumi hufananisha Wakristo wote walio katika mstari wa kupata au wanaodai kuwa katika mstari wa kupata Ufalme wa mbinguni. Ilikuwa kwenye Pentekoste 33 W.K. kwamba kundi la Kikristo liliahidiwa ndoa kwa Yesu Kristo, Bwana-arusi aliyefufuliwa na kutukuzwa. Lakini ndoa ilikuwa ifanyike mbinguni wakati fulani ujao usioonyeshwa waziwazi.

Katika kielezi hicho, wale wanawali kumi hutoka na kwenda nje kwa kusudi la kukaribisha bwana-arusi na kujiunga katika mwandamano wa arusi. Awasilipo, wataangaza njia ya mwandamano kwa taa zao, hivyo kumheshimu aletapo bibi-arusi wake kwenye nyumba aliyotarishiwa. Hata hivyo, Yesu anaeleza hivi: “Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.”

Ukawivu mwendelevu wa bwana-arusi huonyesha kwamba kuwapo kwa Kristo akiwa Mfalme anayetawala kungekuwa katika wakati ujao ulio mbali. Hatimaye anakuja kwenye kiti chake cha ufalme katika mwaka 1914. Wakati wa ule usiku mrefu kabla ya hapo, wale wanawali wote wanalala usingizi. Lakini hawakushutumiwa kwa sababu hiyo. Wale wanawali wapumbavu wanashutumiwa kwa kutokuwa na mafuta kwa ajili ya vyombo vyao. Yesu aeleza namna wale wanawali wanavyoamka kabla ya bwana-arusi kuwasili:

“Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.”

Mafuta yafananisha kile kinachowaendeleza Wakristo wakiwa wanaangaza wakiwa vimulikaji, yaani, Neno la Mungu lililovuviwa, ambalo wanashika sana, pamoja na roho takatifu, ambayo husaidia katika kuelewa Neno hilo. Mafuta hayo ya kiroho huwezesha wale wanawali wenye busara waangaze nuru katika kumkaribisha bwana-arusi wakati wa mwandamano wa kwenda kwenye karamu ya arusi. Lakini jamii ya wale wanawali wapumbavu haina ndani yao, katika vyombo vyao, yale mafuta ya kiroho yanayohita-jiwa. Kwa hiyo Yesu aeleza linalotukia:

“Na hao [wanawali wapumbavu] walipokuwa wakienda kununua [mafuta], bwana arusi akaja, nao [wanawali] waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.”

Baada ya Kristo kuwasili katika Ufalme wake wa kimbingu, jamii ya wale wanawali wenye busara ya Wakristo wa kweli wapakwa-mafuta waliamuka kwenye pendeleo lao la kuangaza nuru katika ulimwengu huu uliotiwa giza katika kusifu Bwana-arusi aliyerudi. Lakini wale waliofananishwa na wale wanawali wapumbavu walikuwa hawako tayari kuandaa sifa hii ya kukaribisha. Kwa hiyo wakati ufikapo, Kristo hawafungulii mlango wa karamu ya arusi mbinguni. Yeye awaacha nje katika weusi wa usiku mzito zaidi ya wote wa ulimwengu, wakapotee na wafanya kazi wengine wote wa uasi-sheria. “Basi kesheni,” Yesu amalizia, “kwa sababu hamjui siku wala saa.” Mathayo 25:1-13.

◆ Ni nani wanafananishwa na wale wanawali kumi?

◆ Ahadi ya ndoa kwa bwana-arusi yafanywa wakati gani, lakini yeye awasili wakati gani apeleke bibi-arusi wake kwenye karamu ya arusi?

◆ Mafuta yawakilisha nini, na kuwa nayo kwawezesha wale wanawali wenye busara kufanya nini?

◆ Karamu ya arusi inatukia wapi?

◆ Wale wanawali wapumbavu wakosa thawabu gani tukufu, nao wapatwa na nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki