Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 1/1 uku. 32
  • Kutolewa kwa Hati-Kunjo za Baharifu za Mwisho

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutolewa kwa Hati-Kunjo za Baharifu za Mwisho
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 1/1 uku. 32

Kutolewa kwa Hati-Kunjo za Baharifu za Mwisho

SEPTEMBA iliyopita kizuizi cha kiwanachuo kilichokuwako kwa miongo mingi kiliondolewa hatimaye. Mabishano makali kati ya wanafunzi wa Hati-Kunjo za Baharifu yalionekana kana kwamba yameisha, ingawa huenda ikawa mabishano mapya yameanza.

Hati-kunjo za Baharifu zilivumbuliwa katika mapango karibu na Baharifu katika 1947 na katika miaka iliyofuata. Zilikuwa zenye thamani sana katika kuonyesha usahihi wa maandishiasilia ya Maandiko ya Kiebrania na katika kuangaza nuru kwenye hali za kidini katika Palestina wakati Yesu alipokuwa duniani. (Isaya 40:8) Ingawa hati-mkono fulani zilitangazwa kwa chapa haraka, katika 1991 hati-mkono karibu 400 bado hazikuwa zimetangazwa kwa chapa na hazikupatikana kwa wanachuo walio wengi. Wengi walihisi kama Profesa Ben Zion Wacholder, “aliyefadhaishwa na ufahamu kwamba kwa mwendo wa sasa wa kutangaza kwa chapa sisi sote tutakuwa tumekufa wakati maandishiasilia yote ya Baharifu yatakapopatikana kwa ulimwengu.”

Lakini hali hiyo ilibadilika Septemba iliyopita. Kwanza, Profesa Wacholder na mshirika mmoja, Martin Abegg, walitangaza kwamba walikuwa wametumia kompyuta kwa ustadi kutokeza upya maandishi hayo yenye kulindwa kwa ukaribu. Kisha, Maktaba ya Huntington katika San Marino, California, U.S.A., ilitangaza kwamba ilikuwa na picha za hati-mkono za awali na kwamba ingefanya zipatikane kwa wanachuo mashuhuri bila kuzuiwa. Yaonekana, nakala kadhaa za foto za hati-kunjo hizo zilikuwa zimefanywa ili kuhakikisha kwamba zinahifadhiwa. Seti za foto hizo zilikuwa zimewekwa akibani katika mahali tofauti-tofauti, na seti moja ilikuja hatimaye kuwa katika Maktaba ya Huntington.

Mwanachuo mmoja alikuita kubadilika huko kwa mambo ‘hali ya kiwanachuo iliyo sawa na kuvunja Ukuta wa Berlin.’ Wahariri waliowekwa rasmi walikuita kule kutangaza kwa chapa kwa maandishiasilia hayo yaliyotolewa kwa kompyuta na pia kutoa kwa foto hizo ‘kuiba.’ Yaelekea, kutakuwako mabishano kwa miaka mingi juu ya uhalali wa hilo. Kwa sasa, yaonekana kwamba wanachuo wengine zaidi wataweza hatimaye kuchunguza maandishi yote ya Hati-Kunjo za Baharifu.

[Picha katika ukurasa wa 32]

Nakala ya maelezo juu ya Habakuki, moja ya zile Hati-Kunjo za Baharifu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki